Tuesday , 16 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Ripoti kikosi kazi kutinga kwa Rais Samia kesho
Habari za SiasaTangulizi

Ripoti kikosi kazi kutinga kwa Rais Samia kesho

Zitto Kabwe, Kiongozi wa ACT Wazalendo
Spread the love

 

RAIS Samia Suluhu Hassan, amesema kesho Ijumaa, tarehe 21 Oktoba 2022, atapokea ripoti ya kikosi kazi alichokiunda kuratibu maoni ya wadau wa demokrasia ya vyama vingi vya siasa, ambayo itafanyiwa kazi mara moja. Anaripoti Regina Mkonde, Dar es Salaam … (endelea).

Mkuu huyo wa nchi ametoa taarifa hiyo leo Alhamisi, tarehe 20 Oktoba 2022, jijini Dar es Salaam akizungumza katika maadhimisho ya miaka 25 ya Shirika la Wanawake katika Sheria na Maendeleo barani Afrika (WiLDAF), tawi la Tanzania.

Rais Samia amesema, kupitia ripoti hiyo atapokea mapendekezo ya vyama vya siasa kuhusu namna ya kuboresha sheria za uchaguzi na vyama hivyo, kwa ajili ya kuongeza ushiriki wa wanawake kwenye masuala ya uchaguzi.

Rais Samia Suluhu Hassan

“Kama mnavyoelewa hivi karibuni na infact ni kesho natarajia kupokea ripoti ya kikosi kazi cha vyama niliyounda na katika ripoti ile nategemea vyama vya siasa watakuja sababu wameninong’oneza nilipokutana nao, kuwa watakuja na mapendekezo ya maberekebisho ya sheria ya uchaguzi na vyama vya siasa,” amesema Rais Samia na kuongeza:

“Niwahakikishie Serikali itayafanyia kazi mara moja pamoja na ile kazi inayofanywa sasa hivi na Tume ya Kurekebisha Sheria kuangalia maeneo ambayo wadau wa sheria wameyaonesha.”

Kikosi hicho kilicho chini ya Mwenyekiti, Profesa Rwekaza Mukandala, kinawasilisha ripoti hiyo baada ya kupokea maoni kutoka wadau mbalimbali, ikiwemo viongozi wa Serikali wastaafu akiwemo Rais Mstaafu, Jakaya Kikwete. Viongozi wa dini, asasi za kiraia, vyama vya siasa na viongozi wa dini.

Kikosi hicho cha chenye wajumbe 25 ambao wanaripoti moja kwa moja kwa Rais, kiliundwa Novemba mwaka jana na kuanza rasmi zoezi la kupokea maoni Aprili, 2022 na kufungwa rasmi Septemba mwaka huu.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Rais Samia amfariji mjane wa Musa Abdulrahman

Spread the loveRais Samia Suluhu Hassan leo Jumanne amempa pole Mwanakheri Mussa...

Habari za Siasa

Nape: Wanasiasa, wanahabari, wafanyabiashara mteteeni Samia

Spread the loveWaziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari na Mawasiliano,...

Habari za Siasa

CAG: TAWA imegawa vibali vya uwindaji bila idhini ya waziri

Spread the loveRIPOTI ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali...

Habari za Siasa

TAMISEMI yatenga bil. 17.79 kwa ajili uchaguzi serikali za mitaa

Spread the loveWIZARA Ofisi ya Rais-TAMISEMI, imetenga fedha kiasi cha Sh. 17.79...

error: Content is protected !!