Wednesday , 1 May 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Kapinga awataka wananchi kutunza miundombinu ya umeme
Habari za Siasa

Kapinga awataka wananchi kutunza miundombinu ya umeme

Spread the love

Naibu Waziri wa Nishati, Judith Kapinga amewataka wananchi kuhakikisha wanalinda na kutunza miundombinu ya umeme nchini ili itumike kwa muda mrefu. Anaripoti Mwandishi Wetu …(endelea).

Amesema hayo leo tarehe 29 Novemba 2023 mkoani Morogoro wakati akiwasha umeme kwa mara ya kwanza katika vijiji vya Maseyu na Newland vilivyopo katika Kata ya Gwata katika ziara yake ya kukagua utejekezaji wa miradi ya Wakala wa Nishati Vijijini (REA) mkoani humo.

Amesema serikali imekuwa ikitumia fedha nyingi katika utekelezaji wa miradi ya kusambaza umeme vijijini lengo likiwa ni kuharakisha maendelea, hivyo wanapaswa kusaidia kulinda miundimbinu hiyo ili iwanufaishe wananchi wengi na kwa muda mrefu.

“Msiruhusu upenyo wa mtu kuhujumu miundombinu, tuhakikishe tunailinda kwani serikali imewekeza fedha nyingi na tuipe thamani inayostahili” amesema Naibu Waziri Kapinga wakati akizungumza na wananchi wa vijiji vya Maseyu na Newland mkoani Morogoro.

Amesema serikali imejipambanua kwa kuwaletea wananchi maendeleo kwa kuweka miundombinu wezweshi ili waweze kushiriki shughuli mbali mbali za uchumi.

Naibu Waziri Kapinga amewataka wakandarasi wanaojenga miradi ya REA kuhakikisha wanaikamilisha kwa wakati ili ifikapo Juni 2024 miradi yote iwe imekamilika.

Akielezea utekelezaji wa miradi, Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa REA, Mhandisi Jones Olotu amesema serikali imewekeza  jumla ya Sh 114.6 billioni kwa miradi mitano inayotekelezwa  kwa mkoa wa Morogoro.

Amesema Serikali kupitia REA inaendelea kutekeleza miradi mbalimbali nchi nzima pamoja na kuwasimamia kwa karibu wakandarasi wote waliopewa zabuni yakutekeleza miradi mbalimbali ya umeme ili kuhakikisha miradi hiyo inakamilika kwa wakati na kwa ubora uliopangwa.

Mhandisi Olotu amesema mkoa wa Morogoro una jumla ya vijiji 669 ambapo hadi kufikia sasa vijiji 583 sawa na asilimia 87.1% vimepata huduma ya umeme kupitia mitano

Ameitaja miradi hiyo kuwa ni REA Awamu ya Tatu Mzunguko wa Pili (REA III Round II), Mradi wa Kituo cha Kupoozea Umeme cha Ifakara, Mradi wa ujazilizi (Densification IIB), Mradi wa Kupeleka umeme kwenye migodi midogo na maeneo ya kilimo na Mradi wa Kupeleka umeme kwenye Vituo vya Afya na Pampu za Maji.

Kwa upande wake, Mbunge wa Morogoro Kusini Mashariki, Khamis Taletale aliishukuru serikali kwa  utekelezaji wa kwa kutoa fedha za kutosha kwa ajili ya utekelezaji wa miradi ya nishati vijini jimboni kwake.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Mavunde ataja malengo “Vision 2030”

Spread the loveWAZIRI wa Madini amesema dhana ya “Vision 2030” inakusudia kuiendeleza...

Habari za Siasa

Mavunde aomba bilioni 231.9 bajeti wizara ya madini

Spread the loveWAZIRI wa Madini, Anthony Mavunde leo Jumanne amewasilisha hotuba ya...

Habari za SiasaTangulizi

Lissu amjibu Fatma Karume kuhusu Rais Samia

Spread the love  MAKAMU Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema)...

Habari za SiasaTangulizi

Dk. Slaa: Watanzania iungeni mkono Chadema uchaguzi 2025

Spread the loveMWANASIASA mkongwe nchini Tanzania, Dk. Wilbroad Slaa, amewataka watanzania wakiunge...

error: Content is protected !!