December 9, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Kanisa kumfanyia maombi Rais Magufuli  

Rais John Magufuli

Spread the love

KANISA la Tanzania Fellowship imekusudia kufanya maombi maalumu ya siku nne ya kuliombea Taifa, Rais Dk John Magufuli  na watendaji wake kwa ajili ya kuhamia Makao Makuu ya Serikali mkoani Dodoma. Anaripoti Danson Kaijage, Dodoma … (endelea).

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Askofu Mkuu wa Kanisa la Tanzania Fellowship Dk. Godfrey Malassy amesema kuwa, maombi hayo maalumu ni kwa ajili ya ujio wake na watendaji mbalimbali.

Amesema, pamoja na kuombea ujio huo pia yatalenga kusaidia serikali kuongoza na kusimamia maamuzi yatakayoweza kuleta maendeleo kwa Watanzania bila itikadi yoyote ya kidini.

“Ukizingatia hata mwenyewe Rais amekuwa na maombi ya kuwaomba Watanzania kumwombea ili aweze kufanikiwa mahitaji yake kwa ajili ya Taifa hili la Tanzania,” amesema.

“Pia ni imani yetu kwa siku hizi nne za maombi hayo pia yatasaidia kuvunja nguvu ya shetani ili zisiweze kutawala makao makuu ya nchi ambapo kwa hivi sasa serikali imeamua kuhamishia makao makuu yake hapa,” amesema Dk. Malassy.

Aidha, amewataka Watanzania kuunga mkono yale ambayo serikali ya awamu ya tano imeweza kufanikiwa kwa kuyaombea ili yaweze kuleta mabadiliko kwa Taifa hili.

“Kuna mengi ya kuyaombea kama vile kwa upande wa miradi ambayo tayari imeonekana na ile ambayo ipo mbioni kufanikisha ikiwemo ndege zinazomilikiwa na Shirika la Ndege la ATCL na ujenzi wa reli ya kisasa,” amesema.

Katika kipindi cha miaka mitatu ya Rais Magufuli amefanikiwa kuimarisha nidhamu, uadilifu na uwajibikaji ndani ya utumishi wa umma pamoja na kukemea uzembe na kujenga ari ya kufanya kazi haya yote yanahitajika kuendelea kuombewa.

Askofu huyo hata hivyo ametaja malengo mengine ya kufanya maombi hayo ni kuhakikisha pia taifa linafikia mafanikio ya kutimiza ndoto zake za kuwaongoza watanzania katika uchumi wa viwanda vya kati.

Dk. Malassy pia amewashauri watendaji wake wa serikali kuhakikisha wanajisimamia katika nafasi zao kwa uaminifu ili waweze kuaminiwa kama ilivyo kwa Rais ambaye anakubalika karibu watanzania walio wengi.

Amesema ili kuhakikisha tunafanikiwa makanisa na watanzania kwa ujumla wahakikishe wanaendelea kujikita kwa kumwombea Rais bila kukoma ikiwa na pamoja na Taifa na serikali

Katika kongamano hilo ambalo ni la siku nne lililowashiriksha maaskofu,wachungaji,wainjilisti,wazee wa kanisa na waumini kutoka mikoa mbalimbali.

error: Content is protected !!