Saturday , 20 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Mshahara wa Lissu, sasa kaa la moto
Habari za SiasaTangulizi

Mshahara wa Lissu, sasa kaa la moto

Spread the love

MJADALA juu ya kusimamishwa mshahara wa Mbunge wa Singida Mashariki (Chadema), Tundu Lissu, umezidi kupamba moto. Anaripoti Faki Sosi … (endelea).

Lissu ambaye yuko nchini Ubelgiji anakoendelea na matibabu yake, yuko katika hatari ya kuzuiwa mshahara wake na hata kutenguliwa ubunge wake.

Akizungumza bungeni jana asubuhi, tarehe 7 Februari 2019, Spika wa Bunge la Jamhuri, Job Ndugai alisema, hafahamu kama Lissu ni mgonjwa ama ameshapona.

Alisema, kutokana na hali hiyo, anafikiria kuzuia mshahara wa mwanasiasa huyo, pamoja na stahili zake nyingine.

Alisema, hata yeye hafahamu mahali ambako Lissu alipo na wala hajui kama amepona ama bado anaendelea na matibabu.

“Haya mambo yapo ndani ya uwezo wangu. Kuna hoja hapa tena ya msingi, kwamba mbunge hayupo bungeni. Hayupo hospitali. Anazurula ulimwenguni kuchafua serikali. Nafikiri tunaweza kusimamisha malipo yake, hadi hapo tutakapo pata taarifa zake.”

Spika Ndugai alikuwa alitoa kauli hiyo, wakati akijibu swali la mbunge wa mbunge wa Geita Vijijini (CCM), Joseph Kasheku Msukuma.

Lissu aliyeshambuliwa kwa risasi akiwa nyumbani kwake, Area ‘D’ mjini Dodoma, tarehe 7 Septemba mwaka 2017, anapatiwa matibabu na madaktari bingwa wa mifupa katika hospitali ya chuo kikuu cha Luvein, kilichopo nchini Ubelgiji.

Akizungumza na MwanaHALISI Online, mchambuzi wa masauala ya siasa za ndani na nje ya nchi na mwanazuoni mashuhuri nchini, Dk. Azaveri Lwaitama amesema, Spika Ndugai na Bunge lenyewe, halipaswi kuwa na haraka kufanya maamuzi hayo.

Alisema, kwa taarifa alizonazo, Lissu bado ni mgonjwa na anaendelea na matibabu yake nchini Ubelgiji na mara atakapomaliza, atarejea nchini.

Anasema, “itakuwa ni aibu na fedheha kubwa kwa Bunge na taifa kuzuia mshahara wa Lissu kwa sababu tu hayuko bungeni na Spika Ndugai, hafahamu kama amepona ama bado ni mgonjwa. Ni ushauri wangu, Bunge lisijiingize kwenye fedhea hiyo.”

Anasema, “Lissu ni mgonjwa na mshahara wake utakoma pale tu, atakapokoma kuwa mbunge.  Ni aibu kubwa kwa Bunge kuruhusu mbunge wake aliyepigwa risasi mchana kweupe, na ambaye anajua kuwa yupo nje kwa matibabu; na hajapokea barua yoyote ya daktari kuwa mbunge amepona anazuia mshahara wake.”

Amesema kuwa  sio ajabu Lissu kuzungumza na vyombo vya habari. “ Lissu alizungumza na vyombo vya habari akiwa Nairobi kwenye matibabu. Alizungumza na vyombo vya habari akiwa hospitalini Ubelgiji anazungumza sasa ulimwenguni anakotembelea.”

“Hata angekuwa mtu mwingine yeyote asingeweza kukaa kimya kwa tukio lile. Kama yeye mbunge amepigwa risasi mchana kweupe, nani aliyeko salama,” anahoji Dk. Lwaitama.

Anamshauri Spika Ndugai kumsubiri Lissu arudi nchini akiwa na vielelezo vya matibabu yake.

Anaongeza: “Wapi imeandikwa mgonjwa haruhusiwa kutembea akiwa anafanya mazoezi na matembezi  huku akisubiri matibabu mengine?”

Naye Dk. Benson Bana, anasema kuwa tukio la kupigwa risasi Lissu limemsikitisha na kwamba amelisihi bunge kutathimini mazingira ya tukio hilo.

Hata hivyo, Dk. Bana anasema, Bunge lina kanuni zake juu ya watumishi wake, na kwamba wanaweza kuzitumia kumsimamishia mshara mtumishi ambaye amekiuka taratibu.

Amesema, “…ni vema wabunge na spika waliangalie kwa uzito unaostahili suala hili la Lissu.”

Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu nchini (HLRC), Anna Henga amesema, sio halali kwa mbunge ambaye bado hajakoma kuwa mbunge kukatishiwa mshahara wake.

Amesema, “Lissu bado ni mbunge. Hivyo basi, huwezi kwa namna yeyote ile kuzuia mshahara wake. Huyu bado anahaki zote kama mbunge ya kupata mshahara  na stahki zake nyingine.”

Kwa mujibu wa Kanuni za Bunge, mbunge wa Bunge la Jamhuri, anaweza kusita kushika nafasi hiyo, iwapo atashindwa kuhudhuria mikutano mitatu mfululizo na bila kuwapo kwa taarifa.

Hakuna kokote kwenye Kanuni za Bunge, kunakotoa mamlaka kwa Spika kusitisha mshahara wa mbunge yeyote.

“Mbunge aweza kusimamishwa ubunge kwa azimio la Bunge. Siyo matakwa binafsi ya Spika. Hakuna ambaye hafahamu mahali ambako Lissu yupo,” ameeleza John Mnyika, mbunge wa Kibamba na Naibu Katibu Mkuu wa Chadema, Tanzania Bara.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

BiasharaHabari za Siasa

Mavunde aagiza Perseus kuharakisha fidia Sengerema

Spread the loveWaziri wa Madini, Anthony Mavunde ameipongeza Kampuni ya Perseus kwa...

Habari za Siasa

Kigogo Chadema awanyooshea vidole vigogo serikalini kuhusu ripoti ya CAG

Spread the love  MWANACHAMA wa Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Boniface Jacob, amedai...

Habari za Siasa

Wabunge waikalia kooni TAKUKURU Bungeni

Spread the love  BAADHI ya wabunge wamelia na changamoto za utendaji wa...

Habari za SiasaTangulizi

Mpina ataka Waziri Majaliwa ajiuzulu, akosoa teuzi za mawaziri

Spread the love  MBUNGE wa Kisesa, Luhaga Mpina, amemtaka Waziri Mkuu, Kassim...

error: Content is protected !!