March 2, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Kamati ya Bunge yaonesha huruma kwa wananchi  

Waziri Kivuli wa Fedha na Uchumi, James Mbatia

Spread the love

WABUNGE wamejadili na kupitisha miswada miwili ukiwamo wa Sheria ya Mamlaka ya Udhibiti Usafiri wa Ardhini, huku kamati ya Bunge ikikataa kiwango cha adhabu na vifungo vikubwa kwenye sheria hiyo na kushauri vipunguzwe ili kuendana na hali halisi. Anaripoti Danson Kaijage…(endelea).

Viwango vya tozo vinavyopigiwa kelele ili vipunguzwe ni vile vinavyohusu adhabu kwa watumiaji wa huduma za usafiri wa ardhini.

Muswada huo una kifungu cha 42 (1) na (2) kinachotoa adhabu kubwa ya faini na kifungo kwa mtu aliyetenda kosa cha Sh. 3,000,000 kwa mtu mmoja na Sh. 5,000,000 kwa kampuni au kifungo cha miaka miwili jela au vyote kwa pamoja.

Akiwasilisha maoni na ushauri wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundo Mbinu kuhusu muswada huo leo tarehe 30 Januari 2019, Dk. Chuachua Mohamed Rashid amesema, kamati hiyo inaona asilimia 1.5 inayotozwa kwenye pato ghafi ni kiwango kikubwa sana, kwani wakati mwingine unaweza kukusanya kiasi kingi, lakini kwa uhalisia hakuna faida kubwa.

Kwa mujibu wa Chuachua, kamati yao inapendekeza kiwango hicho cha asilimia 1.5 kirekebishwe na kiwe asilimia moja kwenye kifungu cha 35 (3) ambacho kinazungumzia tozo katika sheria hiyo.

“Katika maoni yetu ya jumla, kamati inaona viwango vya tozo za watoa huduma kubadilisha tozo ni mlolongo mrefu na kwa muda mrefu viwango hivyo havijafanyiwa marekebisho.

“Tunashauri katika kanuni kuwe na kikokotoo kinachotokana na gharama ya uendeshaji ili kutatua changamoto hii,”amesema.

James Mbatia, Msemaji wa Kambi Rasmi ya Upinzani bungeni akiwasilisha maoni na ushauri kuhusu tozo na adhabu mbalimbali zilizotajwa katika muswada huo, amesema lengo la muswada huo lisiwe ni kuwatesa au kuwapa adhabu watumiaji wa huduma za usafiri wa ardhini.

Katika muswada huo, Mbatia alianza kwa kuunga mkono serikali kuleta bungeni muswada huo akidai kuwa una maslahi mapana kwa taifa na wala wao hawaupingi.

“Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni inashauri kwamba adhabu ni kubwa mno na kinatoa taswira ya kukomoa badala ya kurekebisha tabia.

“Kwa ajili ya kuweka mazingira rafiki ili watu wote waweze kunufaika na mwenendo wa soko na kuondoa uwezekano wa baadhi ya watu kuhodhi mwenendo wa soko na ni vyema serikali iweke utaratibu wa kulinda wadau wote,” amesema Mbatia.

error: Content is protected !!