October 2, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Kakolanya aishika pabaya Yanga

Makao Makuu ya Klabu ya Yanga

Spread the love

UONGOZI wa klabu ya Yanga umekili kupokea barua kutoka kwa mwanasheria wa mlinda mlango wao Benno Kakolanya kutaka kuvunja mkataba na timu hiyo licha ya kulipwa stahiki zake zote alizokuwa akidai hapo awali. Anaripoti Kelvin mwaipungu… (endelea)

Kaimu M/nyekiti wa klabu hiyo Samuel Lukumay alikili uongozi wa klabu hiyo kupokea barua ya pili kutoka kwa mchezaji huyo 28 january, 2019 ambayo alikuwa akisisitiza kutaka kuvunja mkataba na timu hiyo licha ya kulipwa stahiki zake zote.

“Benno aliuandikia uongozi barua ya siku 14 ambayo ilikuwa ni ‘notice’ kumlipa haki zake au kuvunja mkataba kama uongozi ilibidi kufanya juhudi ili kumlipa stahiki zake kama ambavyo tunawalipa wachezaji wenzake na Benno akawa amelipwa madai yake yote na tumewajibu wanasheria wake kwa barua kuwa kile alichokuwa anadai tumeshamlipa”

“Tulichokipata tena kutoka kwa wanasheria wake ni barua ya msisitizo wa kutaka kuvunja mkataba ambayo tumeipata siku ya jana” alisema Lukumay

Ikumbukwe Benno ameingia kwenye mgogoro na klabu hiyo baada ya kutaka kulipwa mshahara wake wa miezi mitatu pamoja na fedha ya usajiri ambayo hakumaliziwa kiasi cha kususa kuingia kambini wakati timu hiyo ikijiandaa na mchezo wa Ligi Kuu dhidi ya Mwadui Fc.

Baada ya mchezaji huyo kutoripoti kambini kocha mkuu wa klabu hiyo Mwinyi Zahera alisema kuwa hamhitaji tena mchezaji huyo ndani ya kikosi chake licha ya kulipwa stahiki zake zote kwa kuwa anaweza kuleta mpasuko ndani ya timu kwa kuwa wachezaji wanaodai ni wengi.

Kwa sasa klabu ya Yanga ina hali ngumu ya kifedha toka alipojihudhulu  aliyekuwa M/nyekiti wa klabu hiyo Yusuph Manji ambae pia alikuwa kama mfadhili mkuu.

 

error: Content is protected !!