Friday , 26 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Kada CCM atafuna pesa za wafanyabiashara
Habari za Siasa

Kada CCM atafuna pesa za wafanyabiashara

Spread the love

MKUU wa Mkoa wa Mwanza, John Mongella amemtaka kada wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Joseph Kahungwa kurejesha mara moja pesa zilizochangwa na wadau mkoani humo kwa ajili ya kuanzisha benki ya “Mwanza Community Bank” zilizochangwa tangu mwaka 2013. Anaripoti Moses Mseti, Mwanza … (endelea).

Kahungwa ambaye aliwahi kuingia katika kinyang`anyiro cha kuwania ubunge ndani ya CCM mwaka 2015 jimbo la Nyamagana  pia ni Makamu Mwenyekiti wa chama cha wenye biashara, viwanda na wakulima (TCCIA) Taifa.

Kahungwa pamoja na viongozi wenzake wanakabiliwa na tuhuma hizo za upigaji wa fedha kiasi kadiriwa kufikia milioni mia tano.

Tangu mwaka 2013 Kahungwa na viongozi wenzake ambao waliteuliwa kusimamia zoezi la uanzishwaji wa benki hiyo ya wana mwanza walishindwa uianzishaji wake kutokana na kwamba fedha za kuanzisha benki hiyo hazijatosha.

Taarifa za Kahungwa kushtumiwa kupiga pesa zimeibuliwa leo katika kikao cha wadau wa biashara mkoa wa Mwanza kilichosimamiwa na mkuu wa mkoa huo.

Katika kikao hicho ambacho kilianza kwa uwasilishwaji wa taarifa mbalimbali, ambapo ilipofika ajenda hiyo, ndipo Mongella alipohoji kuhusu uanzishwaji wa benki hiyo ambayo mikakati yake ilianza mwaka 2012/13.

Akizungumza katika kikao hicho, Mongella alisema kwa taarifa alizonazo ofisini kwake zinatia shaka hela zilizotolewa na wadau hao kama bado zipo kwa kuwa amekuwa akipokea malalamiko kuhusu pesa hizo.

“Kuna siku tutaamka hapa tutakutana na mshikemshike na wengine hapa ni ndugu zetu nasema tutaanza kukamatana bila sababu.

“Iteni kikao hao watu ambao walitoa hela zao warejeshewe kwa kuwa hili suala nimekuja hapa nimelikuta na naweza kuondoka nikaliacha, nina taarifa hakuna fedha na kama mnakataa ipo siku litaibuka.

“Ras (Katibu tawala mkoa) chukua hili suala muanze kulifanyia kazi, na mwishoni mwa mwezi Julai niwe nimepataa taarifa zake hayo mambo ya wadau wanaotafutwa kuongezea fedha imebaki hadidhi tu hapa,” alisema Mongella.

Mongella aliwashauri viongozi wote wanaohusika na zoezi la uanzishwaji wa benki hiyo, kukaa chini na kuchukua hatua ya kurudishia hela zao.

Kwa upande wake, Joseph Kahungwa ambaye kwa muda mrefu amekuwa akikabiliwa na tuhuma hizo za upigaji wa fedha za wadau hao amedai fedha hizo zipo.

Kahungwa alisema fedha zilizotolewa na wadau hao zimehifadhiwa katika benki ya Azania na kwamba bado wanaendelea kutafuta watu wengine ili kuongezea fedha ili kuanzisha benki hiyo.

“Mtaji bado haujatosha ila fedha zao zipo benki ya Azania na sasa tunaendelea kuwatafuta wadau wengine kuongezea fedha ili tuianzishe mara moja,” alisema Kahungwa.

Sanjari na hayo mkuu huyo wa mkoaamemuagiza katibu tawala mkoa wa mwanza Christopher Kadio,  kumvua madaraka Afisa biashara mkoa wa Mwanza Anthony Yesaya kutokana na kushindwa kusimamia vyema uratibu wa mabaraza hayo.

Mongella alisema tangu mwaka 2013 afisa biashara huyo ameshindwa kusimamia vyema kufanyika kwa mabaraza ya biashara ya wilaya na kusababisha vikao vingi kushindwa kufanyika.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Prof. Muhongo akomalia matumizi nishati jadidifu kuondoa uhaba wa umeme

Spread the love  MBUNGE wa Musoma Vijijini (CCM), Profesa Sospeter Muhongo, ameendelea...

Habari za Siasa

Kilosa yawa mfano wa kuigwa miradi ya Mwenge nchini

Spread the love  KIONGOZI wa Mbio za Mwenge Kitaifa Godfrey Mzava amezitaka...

Habari za SiasaTangulizi

Biteko ataja vipaumbele 7 bajeti nishati 2024/25

Spread the love  NAIBU Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Mwekezaji amwaga bil. 39 kujenga viwanda 3 vya uchenjuaji

Spread the loveKampuni ya Mineral Access System Limited (MAST) inayoiwakilishwa kampuni ya...

error: Content is protected !!