Monday , 5 June 2023
Home Gazeti Habari za Siasa Spika Ndugai ‘afyeka’ hotuba ya upinzani
Habari za Siasa

Spika Ndugai ‘afyeka’ hotuba ya upinzani

Job Ndugai, aliyekuwa Spika wa Bunge Tanzania
Spread the love

JOB Ndugai, Spika wa Bunge la Jamhuri, amefyeka baadhi ya vipengele vilivyokuwa ndani ya Hotuba ya Waziri Kivuli wa Wizara ya Fedha na Mipango kwa Mwaka wa Fedha 2019/20. Anaripoti Danson Kaijage, Dodoma…(endelea).

Taarifa ya kufyekwa kwa vipengele hivyo imetolewa na Dk. Tulia Ackson, Naibu Spika akieleza kuwa, Spika Ndugai alitoa maagizo ya kufutwa baadhi ya vipengele na maneno.

Akitoa maelezo hayo leo tarehe 17 Juni 2019, bungeni jijini Dodoma Dk. Ackson amesema kuwa, vipengele vilivyoondolewa katika hotuba hiyo vinatoka katika aya ya 18, 30, 31, 43, 44, 45, 46, 47, 48 49, 50 na 52.

Pia, katika hotuba hiyo kimeondolewa kipengele A chote, I-J aya 104 hadi 110, sehemu A yote aya ya 118 hadi 135, sehemu O aya 147 hadi 148 na sehemu Q yote aya ya 152 hadi 157.

Hotuba hiyo imesomwa leo  na David Silinde, Naibu Waziri Kivuli wa Fedha na Mipango ambapo ameeleza kulalamika hatua ya kufutwa vipengele hivyo bila kupewa taarifa.

Akitoa malalamiko hayo Silinde ameshauri kuwa, ni vema sasa pale kiti cha spika kinapofanya maamuzi, kiwe kinatoa taarifa mapema tofauti na ilivyo sasa.

Hotuba hiyo iliyosomwa leo, ilipaswa kusomwa siku ya bajeti kuu, tarehe 13 Juni 2019, hata hivyo haikusomwa kutokana na kuwa na saini ya Halima Mdee, Waziri Kivuli wa Fedha ambaye anatumikia adhabu ya Bunge.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Lusinde: CCM hatuliachii ng’o jimbo la Moshi Mjini

Spread the loveMJUMBE wa Halmashauri Kuu ya Chama cha Mapinduzi (NEC), Livingston...

Habari za SiasaTangulizi

Serikali ya Mapinduzi Zanzibar: Bakharesa hajavamia shamba letu

Spread the love  IKULU Visiwani Zanzibar, imeeleza kuwa eneo la kiwanda cha...

Habari za SiasaTangulizi

Zanzibar watangaza rasmi kuwa shamba la Razaba ni mali yao

Spread the love  SERIKALI ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ), imetangaza rasmi kwamba shamba...

Habari za SiasaTangulizi

Rais Mwinyi azindua Kamati ya Maridhiano Visiwani

Spread the love  RAIS wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ), Dk. Hussein...

error: Content is protected !!