April 14, 2021

Uhuru hauna Mipaka

NBC yapata tuzo ya utendaji bora

Mkurugenzi wa Fedha wa Benki ya NBC, Peter Nalitolela, akipokea tuzo ya Utendaji Bora kutoka kwa Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa

Spread the love

IMEELEZWA kuwa Benki ya NBC ni benki ya tatu kwa ukubwa nchini Tanzania, hivyo wametunukiwa tuzo ya Utendaji Bora wa sekta ya benki nchini. Anaripoti Danson Kaijage, Dodoma … (endelea).

Akisoma Hotuba Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa NBC, Peter Nalitolela, kwenye kongamano la uwezeshaji 2019 Jijini Dodoma lililofanyika tarehe 15 Juni, 2019 kwenye ukumbi wa mikutano wa Wizara ya Fedha na Mipango, alisema kuwa benki hiyo ni ya tatu kwa ukubwa nchini.

Mbali na kueleza kuwa benki hiyo ni ya tatu kwa ukubwa Tanzania, amesema kuwa hadi kufikia mwezi Machi mwaka huu NBC ilikuwa na mali (ASSET) zenye thamani ya Sh. 1.828 trilioni na amana zenye thamani ya Sh. 1.292 trilioni. 

Aidha kiongozi huyo amesema kuwa mpaka sasa Benki hiyo imeweza kutoa ajira kwa  wafanyakazi wapatao 1200.

Katika hatua nyingine, Nalitolela amesema  kuwa NBC ni kati ya benki kongwe nchini ambayo inaendelea kuwatumikia watanzania kwa zaidi ya miongo mitano kwa uaminifu.

Amesema kwamba NBC ina matawi 51, mashine za kutolea fedha (ATM) 183, mashine za kuchanja (POS) 190 na mawakala zaidi ya 1,400 walioenea nchi nzima.

Kutokana na hali hiyo, leo NBC ikiwakilishwa na Naibu Mkurugenzi wa Fedha wa Benki ya NBC, Peter Nalitolela kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji wa NBC, Theobald Sabi imepokea tuzo kutoka kwa Waziri Mkuu Kassim Majaliwa kwa kutambua utendaji wao wenye ufanisi.

error: Content is protected !!