Saturday , 3 June 2023
Home Gazeti Habari za Siasa Kabendera kukutana na DPP
Habari za Siasa

Kabendera kukutana na DPP

Mwanahabari Erick Kabendera akiingia mahakamani Kisutu
Spread the love

ERICK Kabendera, mwandishi wa habari za uchunguzi ndani na nje ya nchi, ameomba kukutana na Mkurugenzi Mkuu wa Mashtaka nchini (DPP). Anaripoti Faki Sosi…(endelea).

Mbele ya Hakimu Mkazi wa Mahakama Kuu ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam, Agostino Rwizile, Kabendera amekiri mahakamani hapo kuwa ameomba mazungumzo hayo na DPP.

Mwanahabari huyo, anashikiliwa kwenye gereza la Segerea, anakabiliwa na mashitaka matatu ya uhalifu, likiwamo la utakatishaji fedha, ameomba mazungumzo hayo na DPP juu tuhuma zinazomkabili.

Leo Tarehe 11, Oktoba 2019, Mbele ya Hakimu Rwizile, Wakili Jebra Kambole amedai mahakamani hapo, kuwa upande wa washtakiwa umeomba kufungua majadiliano juu ya kusamehewa kwa makosa anayoshitakiwa nayo mahakamani hapo.

Jebra ameileza mahakama, kuwa milango ya majadiliano hayo imefunguliwa kwa kutumia kifungu cha 194 A(2) cha sheria ya mwenendo wa makosa ya jinai  na sharti la kuiarifu mahakama.

Hakimu Rwilize ameahirisha shauri hilo mpaka tarehe 24 Oktoba, 2019.

Makossa mengine anayotuhumiwa nayo Kabandera ni kukwepa kodi kiasi cha sh 173.2 milioni na kushirikiana na genge haramu.

Jumatano, tarehe 1 Oktoba 2019, Kabendera kupitia wakili wake (Wakili Kambole) ameomba msamaha kwa Rais John Magufuli ili kuweza kuwa huru na kuendelea na shughuli zake nyingine.

“Kabendera amemuomba radhi Rais Magufuli, akieleza kwamba kama katika utekelezaji wa majukumu yake ya uanahabari, kuna eneo alifanya makosa au aliteleza, amsamehe ili aweze huru,” alisema Wakili Jebra.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Lusinde: CCM hatuliachii ng’o jimbo la Moshi Mjini

Spread the loveMJUMBE wa Halmashauri Kuu ya Chama cha Mapinduzi (NEC), Livingston...

Habari za SiasaTangulizi

Serikali ya Mapinduzi Zanzibar: Bakharesa hajavamia shamba letu

Spread the love  IKULU Visiwani Zanzibar, imeeleza kuwa eneo la kiwanda cha...

Habari za SiasaTangulizi

Zanzibar watangaza rasmi kuwa shamba la Razaba ni mali yao

Spread the love  SERIKALI ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ), imetangaza rasmi kwamba shamba...

Habari za SiasaTangulizi

Rais Mwinyi azindua Kamati ya Maridhiano Visiwani

Spread the love  RAIS wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ), Dk. Hussein...

error: Content is protected !!