December 3, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Tuzo EJAT zazinduliwa, makundi matatu yatemwa

Kajubi Mukajanga, Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya EJAT

Spread the love

BARAZA la Habari Tanzania (MCT), leo tarehe 11 Oktoba 2019 limezindua rasmi usaili wa kuwania tuzo za umahiri wa uandishi wa habari (EJAT) kwa mwaka 2019. Anaripoti Martin Kamote … (endelea).

Baraza hilo limehimiza waandishi wa habari za mitandao, kujitokeza kwa wingi huku likiongeza makundi matatu mapya ya tuzo na kuwa 20.

Makundi toka 17 ya awali ni habari za hedhi salama, uandishi wa habari za ubunifu na maendeleo ya watu pia habari za afya ya uzazi.

Kajubi Mukajanga, Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya EJAT amesema, makundi yaliyoshindaniwa mwaka jana na sasa hayatokuwepo ni habari za usalama na ubora wa chakula, habari za kodi na mapato pamoja na habari za afya kwa kuwa, yamekosa wadhamini.

Tuzo hizo zimedhaminiwa na Taasisi ya Vyombo vya Habari Kusini mwa Afrika Tawi la Tanzania (MISATAN), Wakfu wa Vyombo vya Habari Tanzania (TMF), Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF), Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake Tanzania (TAMWA).
Wengine ni Umoja wa Klabu za Waandishi wa Habari Tanzania (UTPC), HakiElimu, Sikika, Agriculture Non_State ASctors Forum (ANSAF) na Chama cha Wamiliki wa Vyombo Vya Habari Tanzania (MOAT).
error: Content is protected !!