MAMLAKA ya Hali ya Hewa nchini (TMA), imewataka wananchi kuchukua tahadhari kutokana na kuwepo kwa vipindi vifupi vya mvua kubwa, upepo mkali na mawimbi makubwa, vinavyotarajiwa kujitokeza katika baadhi ya maeneo nchini. Anaripoti Martin Kamote…(endelea).
Pia, imewataka wananchi kuendelea kufuatilia taarifa za hali ya hewa zinazotolewa na mamlaka hiyo, ili kuweza kuwa na habari sahihi kuhusu mabadiliko ya hali ya hewa nchini.
Dk. Agnes Kijazi, Mkurugenzi Mkuu wa TMA amesema, wahati huu wa mvua za vuli, inatarajiwa kuwepo vipindi vifupi vya mvua kubwa na kwamba, mvua zinazoendelea kwa sasa, ni za msimu wa vuli kwa maeneo yanayopata mvua mbili kwa mwaka.
Akieleza utaratibu wa mvua kwa Novemba 2019 hadi Aprili 2020 amesema, wananchi wa mikoa ya Kigoma, Tabora,Rukwa, Katavi, Mbeya, Songwe, Njombe, Iringa, Lindi, Dodoma, Singida, Mtwara na Kusini mwa Mkoa wa Morogoro yanatarajiwa kuwa na mvua za kutosha.
“Wananchi wa maeneo hayo wanapaswa kuzitumia vizuri mvua hizo kwa kupata ushauri kutoka kwa wataalamu wa sekta husika, kwa vile maeneo mengi yanatarajiwa kuwa na mvua za kutosha,” amesema na kuongeza:
“Naendelea kutoa rai kwa wananchi wa mikoa husika kuzitumia mvua hizi kwa kupanda mazao sahihi kwa kufuata ushauri wa wataalamu, kama tunavyoona maeneo mengi yatarajiwa kuwa na mvua za juu ya wastani hadi wastani.”
Leave a comment