Saturday , 27 April 2024
Home Kitengo Maisha Elimu JPM njia panda kuhusu ‘ugaidi Shule za Feza’
ElimuHabari MchanganyikoTangulizi

JPM njia panda kuhusu ‘ugaidi Shule za Feza’

Moja ya shule za Feza zilizopo jijini Dar es Salaam
Spread the love

TUHUMA kuwa Shule za Feza zilizopo hapa nchini zinamilikiwa na watu wanaojihusisha na vitendo vya ugaidi nchini Uturuki na kwamba zinapaswa kufutwa, zinaweza kuiweka serikali ya Tanzania katika njia panda, anaandika Charles William.

Tetesi juu ya wamiliki wa shule hizo kufadhili vikundi vya kigaidi zimekuwepo kwa muda mrefu, hata hivyo uzito wa jambo hilo umeongezeka mapema wiki hii baada ya Rais Recep Erdogan wa Uturuki akiwa ziarani hapa nchini, kuripotiwa kuiomba serikali ya Tanzania kuzifuta shule hizo.

Erdogan ameripotiwa kuiomba Serikali ya Tanzania chini ya Rais John Magufuli kuzifuta Shule za Feza kwasababu Sheikh Fethullah Gullen mmiliki wa shule hizo ni miongoni mwa “wafadhili muhimu” wa mapinduzi yaliyoshindikana Uturuki yakilenga kumng’oa rais huyo madarakani.

Tayari Dk. Augustine Mahiga, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa amenukuliwa akisema, “Serikali ya Uturuki imetoa tuhuma na ushahidi juu ya wamiliki wa shule hizo, na serikali ya Tanzania itachunguza na kutoa uamuzi.”

Hata hivyo, Habibu Miradji ambaye ni Mwenyekiti wa Bodi ya Shule za Feza amesema, “Nina uhakika Serikali haiwezi kuzifunga shule hizo kwasababu itachunguza na kuona ukweli kuwa hatujihusishi na vikundi vya kigaidi.”

Mvutano huu wenye sura ya kisiasa baina ya Rais Erdogan na Sheikh Gullen unaiweka Serikali ya Tanzania ambayo ni ‘mshirika wa karibu’ wa Uturuki katika miradi mbalimbali ya maendeleo katika wakati mgumu wa kuzichukulia hatua shule hizo zenye rekodi nzuri kitaaluma.

Ambapo kutokana na ubora wa elimu inayotolewa katika Shule za Feza baadhi ya viongozi waandamizi wa serikali hapa nchini ni miongoni mwa wazazi wanaosomesha watoto wao katika shule hizo pia.

Ugomvi baina ya Rais Erdogan na Sheikh Gullen unaiweka Serikali ya Tanzania katika nafasi tatanishi ya kuamua kupuuza ubora wa shule hizo na kuzifutia usajili jambo ambalo litapalilia ‘ushirika’ mzuri zaidi na Serikali ya sasa ya Uturuki.

Lakini kwa upande wa pili Tanzania inaweza kuamua kupuuza madai ya Uturuki na kuacha shule hizo ziendelee na shughuli zake, jambo ambalo pia linaweza kuzorotesha uhusiano wa kidiplomasia na Serikali ya Uturuki.

Itakumbukwa kuwa Tanzania imesaini mikataba tisa ya maendeleo na Serikali ya Uturuki ikiwemo inayohusu elimu, tafiti, ujenzi wa reli kwa kiwango cha ‘Standard gauge’ pamoja na usafiri wa anga.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaTangulizi

Prof. Lipumba ajitosa kuviunganisha vyama vya siasa Burundi

Spread the love  MWENYEKITI wa Kituo Cha Demokrasia Tanzania (TCD), Prof. Ibrahim...

Habari Mchanganyiko

Wakili: Ukimpa zawadi mwenza marufuku kumpora hata mkiachana

Spread the love  WANANDOA na watu waliko kwenye mahusiano ya kimapenzi, wamekumbushwa...

Habari Mchanganyiko

Majaliwa: Mvua zimesababisha vifo vya watu 155, kuendelea hadi Mei

Spread the love  WAZIRI Mkuu, Kassim Majaliwa amesema mvua kubwa za El-Nino...

Habari Mchanganyiko

Exim Bank yatoa  vitanda kwa shule ya Jeshi la Polisi Moshi

Spread the love  BENKI ya Exim imekabidhii  seti ya vitanda kwa Shule...

error: Content is protected !!