August 18, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Simba, Yanga warudishwa Uwanja wa Taifa

Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam

Spread the love

HATIMAYE Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye, ameruhusu klabu za Simba na Yanga kuendelea kutumia uwanja wa Taifa, katika michezo yao ya Ligi Kuu Bara baada ya kulidhishwa na ukarabati uliofanyika, anaandika Kelvin Mwaipungu.

Uwanja huo uliofungwa kutokana na uharibifu wa viti uliofanywa na baadhi ya mashabiki walioudhuria katika mchezo huo wa watani wa jadi uliochezwa Oktoba mosi mwaka jana, na kumalizika kwa sare ya 1-1.

Kutokana na uharibifu huo Serikali kupitia Wizara yenye dhamana ya Michezo iliamuru Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) kuzuia mapato yaliopatikana katika mchezo ule mpaka ilipofanyika tasmini na kupata gharama halisi ya ukarabati na kupiga marufuku kwa uwanja huo kutumika tena.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Wizara, uwanja huo utaanza kutumia kuanzia leo, hivyo mchezo wa kesho kati ya Azam na Simba unatarajia kufanyika katika uwanja huo ambao unabeba idadi kubwa ya mashabiki kuliko kulinganisha na ule wa Uhuru ambao uliokuwa unatumika baada ya uwanja wa Taifa kuwa katika marekebisho.

Azam na Simba zimekutana mara 13 katika michezo ya Ligi Kuu, huku Simba ikifanikiwa kupata ushindi katika michezo mitano na Azam FC ikishinda mara 3 na wamefanikiwa kwenda sare mara tano.

Simba ambao kwa sasa ndio vinara wa Ligi Kuu katika msimamo huo ikiwa na alama 45, huku ikifuatiwa kwa ukaribu na Yanga wenye pointi 43 wakishika nafasi ya pili huku Azam wao wakiwa katika nafasi ya nne wakijikusanyia alama 31 baada ya kucheza michezo 19.

error: Content is protected !!