Tuesday , 5 December 2023
Home Gazeti Habari za Siasa JPM azungumzia uchaguzi 2020, aonya wanaopanga kufanya fujo
Habari za Siasa

JPM azungumzia uchaguzi 2020, aonya wanaopanga kufanya fujo

Rais John Magufuli
Spread the love

RAIS John Magufuli amewataka Watanzania kujiandaa vyema, katika kushiriki Uchaguzi Mkuu  wa mwaka huu.Anaripoti Regina Mkonde…(endelea).

Rais Magufuli ametoa wito huo wakati akitoa salamu za kheri ya mwaka mpya kwa Watanzania, leo tarehe 11 Januari 2020, katika ziara yake Visiwani Zanzibar .

“Mwaka huu uwe wa amani na mafanikio, kama mjuavyo baadae mwaka huu nchi yetu inafanya uchaguzi mkuu, hivyo nawasihi wote tujiandae kushiriki uchaguzi huo vizuri. Na bila kusahau kumuomba Mungu aendelee kulilinda na kulisimamia taifa letu,” amesema Rais Magufuli.

Wakati huo huo, Rais Magufuli amewaonya watu wanaopanga kufanya fujo katika uchaguzi huo.

“Ukiona kuna amani ujue kuna watu hawalali, kwa sababu wale ambao wangependa nchi hii isiwe na amani wapo, na vibaraka hawaishi walikuwepo hata enzi za mitume. Hata Mungu aliumba malaika lakini wengine waligoma wakata wawe kama yeye akawafukuza wakawa mashetani.

Kwa hiyo vibaraka wataendelea kuwepo, saa nyingine mnaweza kufanya uchaguzi ukamaliza mwingine akasema nitaapishwa tu, msubiri nitakuja kuapishwa,” ameeleza Rais Magufuli

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Dk. Biteko: Viongozi tuache alama nzuri katika utendaji wetu

Spread the loveNaibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto Biteko...

Habari za SiasaTangulizi

Chanzo maporomoko yaliyoua 65 Hanang, chatajwa

Spread the loveSERIKALI imesema kumeguka kwa sehemu ya Mlima Hanang ambao ilikuwa...

Habari za Siasa

Baba yake Ole Sabaya ashinda Uenyekiti CCM – Arusha

Spread the loveLoy Thomas Sabaya ambaye ni Baba wa aliyekuwa Mkuu wa...

Habari za Siasa

Serikali yaagiza uchunguzi chanzo maporomoko Hanang

Spread the loveSERIKALI imeagiza uchunguzi ufanyike ili kubaini chanzo cha maporomoko ya...

error: Content is protected !!