Sunday , 3 December 2023
Home Gazeti Habari za Siasa JPM amnanga RC aliyemtumbua
Habari za Siasa

JPM amnanga RC aliyemtumbua

Spread the love

RAIS John Magufuli amemnanga Dk. Steven Kebwe, aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Morogoro kwa madai ya ‘kujimegea.’ Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea).

Amesema, alijisahau na baadhi ya miradi kwenye halmashauri ilikuwa yake, akieleza mfano kwamba alipeleka mbao za hoyo kwenye halmashauri moja mkoani humo.

Rais Magufuli ametoa kauli hiyo leo tarehe 20 Novemba 2019, mkoani Morogoro wakati akizungumza na wakazi wa mkoa huo.

Amemsifu mkuu wa mkoa huo wa sasa, ambaye alikuwa Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Mkoa wa Arusha, Loota Sanare kwamba ameanza kazi vizuri.

“…umeanza vizuri, endelea kuchaa kazi. Umeanza vizuri endelea kushughuikia kero zote, nataka niseme wazi, mkuu wa mkoa aliyekuwepo alijisahau.

“Baadhi ya miradi mingine hata kwenye halmashauri ilikuwa yake, kuna halmashauri ali – supply mbao za ovyo, ninayajua yote,” amesema Rais Magufuli.

Akimsife Sanare, Rais Magufuli amesema, ameanza kushughulikia kero za wananchi wa Morogoro na kumwagiza kuendelea kukabili matatizo ya mkoa huo.

“Shughulikia kero za wananchi hawa, shughulikia migogoro ya wafugaji na wakulima, nayo iishe sababu saa nyingine wakati wa kilimo, wakulima wanalima huku wafugaji wanakwenda kulisha mazao.

“Wanapeleka ng’ombe kwenye mazao, nimekuleta uwadhibiti hapa, ili Morogoro iwe na amani, wananchi waishi kwa amani,” amesema.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Dk. Biteko aagiza wakurugenzi TANESCO kukemea rushwa kwenye maeneo yao

Spread the loveNaibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto Biteko...

Habari za SiasaMakala & Uchambuzi

Uongozi wa Samia kuendelea hadi 2030

Spread the loveKWETU sisi tuliowahi kusoma sekondari, iwe O levo au A...

Habari za SiasaMakala & Uchambuzi

Bado askari wastaafu wanaonewa

Spread the loveRAIS wangu Samia Suluhu Hassan tunaendelea kumshukuru Mungu kwamba wote...

Habari za SiasaMakala & Uchambuzi

Tunastawisha ufisadi na kuchukia matunda yake

Spread the loveBUNGE la Jamhuri linaloendelea mjini Dodoma, kwa wiki nzima limetawaliwa...

error: Content is protected !!