December 7, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Jiji la Dodoma kujiendesha kwa mapato ya ndani

Mkurugenzi wa Jiji la Dodoma, Godwin Kunambi

Spread the love

MKURUGENZI  wa Jiji la Dodoma, Godwin Kunambi amesema kuwa jiji hilo linatarajia ifikapo mwaka 2021 jiji hilo litakuwa likijitegemea kwa mapato ya ndani. Anaripoti Dany Tibason, Dodoma … (endelea).

Mbali na hilo alisema  kutokana Dodoma kuwa na ahadi ya kuwa makao makuu pamoja na hadhi ya jiji Dodoma itakuwa jiji la pekee kwa kuwa na vivutio vingi pamoja na mpangilio mzuri wa maeneo mbalimbali ya kupata huduma za kijamii.

Kunambi alitoa kauli hiyo jana alipokuwa ajizungumza na waandishi wa habari kwa lengo la kutoa mwelekeo wa utendaji kazi  unaofanywa na halmashauri ya Jiji la Dodoma.

Katika hatua nyingine, Kunambi alisema kuwa kwa sasa halmashauri ya Jiji la Dodoma ina uwezo wa kukusanya mapato makubwa  ambayo yanatokana na vyanzo vya ndani.

Alisema kuwa katika mwaka wa fedha 2018/19 halmashauri ya jiji la Dodoma iliweka bajeti ya kukusanya kiasi cha Sh. 68  bilioni ambayo ni mapato ya ndani na mpaka sasa imeweza kukusanya Sh. 35 bilioni.

Akielezea hali ya maendeleo katika jiji hilo Kunambi alisema kuwa kwa sasa Jiji la Dodoma halina shida yoyote ya uhaba wa maji wala uhaba wa umeme na kueleza kuwa baada ya muda mfupi miundombinu ya barabara, reli na anga vitakuwa vikifanya kazi.

“Nataka kuwaambia wananchi kuwa Jiji la Dodoma litakuwa jiji la tofauti na majiji mengine yoyote nchini kutokana na kuwa na miundombinu ambayo ni rafiki kwa wakazi wa jiji hilo na rafiki kwa watu wote bila kuepo kwa msongamano kama ilivyo katika majiji mengine.

“Ikumbukwe kuwa wakati mimi nakabidhiwa halmashauri ya Dodoma kabla haijawa jiji 27 Septemba 2016 katika akaunti ya halmashauri nilikuta kiasi cha sh. Milioni 12.7 lakini mpaka sasa kwenye akaunti ya jiji kuna zaidi ya sh. Bilioni 36 kwa michanganuo mbalimbali,” alisema Kunambi.

Akizungumzia suala la elimu Kunambi alisema kuwa kutokana na kuwepo kwa uhaba wa vyumba vya madarasa kwa sasa halmashauri ya jiji imeanzisha ujenzi wa vyumba vya madarasa 20 kwa shule za sekondari na msingi ambavyo vinatarajiwa kukamilika ifikapo mwezi wa tano.

“Tunakiri kuwepo kwa uhaba wa vyumba vya madarasa katika Jiji la Dodoma jambo ambalo limepelekea watoto kushindwa kujiunga katika shule mbalimbali lakini kwa sasa tumeanza kujenga vyumba vya madarasa 20 kutokana na mapato ya ndani ili kuweza kuwafanya watoto watakao chaguliwa kwa awamu ya pili kupata nafasi za kujiunga na shule,” alisema Kunambi.

error: Content is protected !!