MWALIMU ya wa shule ya msingi Medeli ya Jijini Dodoma Anita Kimako (33) mkazi wa Area ‘C’ anayedaiwa kukifungia kabatini kichanga cha miezi mitano na kumjeruhi binti wake wa kazi, anatarajiwa kufikishwa mahakamani kwa tuhuma za kujeruhi huku tuhuma za kukifungia kichanga kabatini zikiendelea kufanyiwa uchunguzi na Jeshi la polisi mkoa wa Dodoma. Anaripoti Dany Tibason, Dodoma … (endelea).
Akizungumza na waandishi wa habari jijini hapa Kamanda wa polisi mkoani Dodoma Kamanda, Gilles Muroto alisema, kuwa mtuhumiwa huyo alikamatwa Desemba 27 mwaka jana kwa kosa la kumshambulia binti wake wa kazi mwenye umri wa miaka 15 (Neema).
Hata hivyo alisema, kitendo cha kumfungia mtoto wa miezi mitano kabati kinachosambaa katika vyombo vya Habari na kwenye mitandao ya kijamii, bado polisi inaendelea kuchunguza ili kubaini ukweli wa tukio hilo.
“Tayari mtuhumiwa ameshahojiwa na mashitaka yanaandaliwa kisha atapelekwa mahakamani kwa kosa la kujeruhi, kuhusu mtoto kufungua kabatini ni kweli mtoto ameonekana ana afya dhaifu lakini bado hatujathibitisha tuhuma hizo tunazifanyia kazi, maana huenda afya ya mtoto ni dhaifu kwa sababu ya kutonyinyeshwa vizuri na mama yake,” alisema Kamanda Muroto.
Akizungumza na waandishi wa Habari juzi akiwa katika hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Dodoma msichana aliyejeruhiwa (Neema) alisema, amekuwa akipigwa mara kwa mara na mwajiri wake (Anita) na kulazimishwa kumnyonyesha mtoto saa nane usiku huku muda mwingine akiwa anahifadhiwa ndani ya kabati.
Mganga mkuu wa hospitali ya Rufaa ya Dodoma, Ernest Ibenzi alisema, binti huyo alipokelewa na mtoto wake siku tatu zilizopita akiwa na majeraha na kumpatia matibabu ambapo kwa sasa anaendelea vizuri huku mtoto huyo kutokana na hali yake mbaya kiafya, walimuanzishia lishe maalum.
Wakati huo alisema, Jeshi hilo limewakamata watuhumiwa wanne kwa kosa la kuvunja stoo nA kuiba mifuko 50 ya saruji huko katika eneo la Chamwino.
Alisema watuhumiwa wamekamatwa wakiwa na gari lenye namba za usajili T 287 APX aina ya Fuso huku akiwataka waliokamatwa kuwa ni Robert Jonas (38) dereva mkazi wa Chamiwno, Lucas Muhombela (18) mkazi wa Chamwino, Shadrack Gabriel (18) mkazi wa Buigiri na Kepha Wenga mkazi wa Buigiri.
Leave a comment