Wednesday , 21 February 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Janeth Rithe ajitosa ngome ya wanawake ACT Wazalendo
Habari za Siasa

Janeth Rithe ajitosa ngome ya wanawake ACT Wazalendo

Janeth Rithe
Spread the love

Katibu wa Habari, Uenezi na Mahusiano na Umma wa chama cha ACT Wazalendo, Janeth Rithe ametangaza rasmi kugombea nafasi ya Uenyekiti wa Ngome ya Wanawake Taifa. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea).

Katika taarifa yake kwa vyombo vya habari iliyotolewa leo tarehe 9 Februari 2024; amesema anagombea nafasi hiyo akiamini anao uwezo, uthubutu na uimara kuongoza ngome hiyo.

Rithe ambaye amekuwa mwenezi wa chama hicho kwa mafanikio makubwa amewaasa wanachama na wanawake wa ACT Wazalendo kwamba hawatojuta endapo watampa ridhaa ya kuongoza Ngome hiyo.

“Nitagombea nafasi ya Uenyekiti wa Ngome ya Wanawake Taifa wa chama chetu katika Uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika tarehe 2 Machi 2024.

“Ninagombea nafasi hii nikijua kabisa kwamba Ngome ya Wanawake inahitaji kiongozi mwenye uthubutu, imara, shupavu na mwenye ushawishi wa kuweza kuunganisha nguvu ya wanawake ndani na nje ya chama kwa maslahi mapana ya Taifa kwa ujumla.

“Niwahakikishie wanawake wa ACT Wazalendo na wanachama kwa ujumla kwamba ninagombea nafasi hii nikiamini ninazo sifa hizo. Hivyo hawatojuta endapo watanipa ridhaa ya kuongoza Ngome ya Wanawake.” amesema Rithe.

Aidha, kupitia taarifa hiyo; Rithe amewaalika waandishi wa habari kuhudhuria mdahalo wa wagombea wa nafasi za Ngome ya Wanawake utakaofanyika tarehe 24 Februari 2024.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Rais Mwinyi ateua waziri wa uchumi na uwekezaji Zanzibar

Spread the loveRAIS wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Dk. Hussein Ali Mwinyi,...

Habari za SiasaTangulizi

Mvua yakatisha mkutano wa Chadema Mbeya

Spread the loveMKUTANO wa hadhara wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema),...

Habari za Siasa

Sugu atumia maandamano ya Chadema kumfikishia ujumbe Spika Tulia

Spread the loveALIYEKUWA Mbunge wa Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi “Sugu”, ametumia maandamano...

Habari za SiasaTangulizi

Sakata la DP World na bandari lafufuka upya

Spread the loveSAKATA la mkataba wa kiserikali kati ya Tanzania na Imarati...

error: Content is protected !!