Saturday , 27 April 2024
Home Habari Mchanganyiko Jamaa aoa pacha watatu wanaofanana “Nawapenda wote
Habari MchanganyikoTangulizi

Jamaa aoa pacha watatu wanaofanana “Nawapenda wote

Spread the love

MWANAUME kutoka Jamhiri ya Kidemokrasia ya Congo ameingia kwenye rekodi ya mfalme Solomoni baada ya kufunga pingu za maisha na mapacha watatu wa kike. Anaripoti Mwandishi Wetu …(endelea).

Mwanaume huyo aliyefahamika kwa jina la Luwizo ambaye ni mkazi wa Kalehe mkoa wa Kivu Kusini nchini DR Congo mapema tarehe 1 Machi mwaka huu alioa mapacha watatu Natasha, Natalie, Nadege katika sherehe ya harusi iliyoelezwa kufana vilivyo.

Katika mahojiano na jarida la AfriMax, Luwizo alifichua kwamba mwanzo Natalie ndiye alikuwa ameuteka moyo wake baada kukutana kwenye mtandao wa kijamii.

Luwizo aliendelea kufunguka kuwa kila alipokuwa kumtembelea Natalie nyumbani kwake na kumkosa, alikuwa akikaribishwa na mmoja wa pacha hao ambao alishindwa kuwatofautisha.

Alisema siku zilipoendelea kusonga, pacha wote watatu walipagawa na penzi lake.

Luwizo alisema alishtuka siku apokutana na wanawake watatu wanaofanana pale alipomtembelea Natalie akitaka waidhinishe ndoa yao. Alisema warembo hao walimwambia wanataka awaoe wote.

“Mwanzoni tulipomwambia kwamba anatakiwa kutuoa sote alishtuka, lakini kwa sababu tayari alikuwa ametupenda sote, hakuna kitu ambacho kiliweza kuzuia mipango yetu kwani pia tulikuwa tunampenda.

“Watu wanaona kuwa haiwezekani kwa wanawake watatu kugawana mume mmoja, lakini kwetu, kugawana kila kitu imekuwa maisha yetu tangu utotoni,” alisema Natalie, mmoja wa mapacha hao watatu.

Akizungumzia tukio hilo Luwizo alisema: “Karibia nizimie. Nikawauliza kati yenu nyote, Natalie ni nani? Wakaniambia nimekutana nao siku tofauti tofauti nilizomtembelea. Nilichanganyikiwa kwani nilikuwa na mpango wa kuoa Natalie lakini kilichonichanganya ni kwamba nisingeweza kuoa mmoja wao na niwaache wale wawili,” alisema na aliongeza kuwa:

“Nililazimika kuwaoa wote kwa sababu ni mapacha watatu. Haukuwa uamuzi rahisi kwa sababu hadi sasa, wazazi wangu hawaelewi ninachofanya”.

Luwizo alibadilishana viapo vya ndoa na pacha hao katika hafla ya faragha iliyohudhuriwa na marafiki wa karibu na familia ingawa wazazi wake hawakuhudhuria harusi hiyo.

“Lazima upoteze kitu ili upate kingine. Isitoshe, mtu ana matakwa yake na namna yake ya kufanya mambo. Kwa hiyo nina furaha kuwaoa hao mapacha watatu bila kujali wengine wanafikiria nini.

“Wazazi wangu walidharau uamuzi wangu ndiyo maana umeona hawakuhudhuria harusi yangu. Lakini ninachoweza kusema mapenzi hayana kikomo,” alisema.

Akizungumzia ndoa yao, Natalie alisema: “Tuna furaha sana. Ndoto yetu ilitimia. Tulifikiri tungetenganishwa na ndoa, lakini Mungu alisikia maombi.”

Aidha, Dada yake Luwizo alisema amefurahishwa na uamuzi wa kaka yake hiyo anaunga mkono uamuzi huo.

“Mwanzoni niliposikia anaoa mapacha watatu sikuelewa lakini baadaye nikaelewa inawezekana, ingawa wazazi wetu walimdharau, nitamuunga mkono kila wakati,” alisema.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaTangulizi

Prof. Lipumba ajitosa kuviunganisha vyama vya siasa Burundi

Spread the love  MWENYEKITI wa Kituo Cha Demokrasia Tanzania (TCD), Prof. Ibrahim...

Habari Mchanganyiko

Wakili: Ukimpa zawadi mwenza marufuku kumpora hata mkiachana

Spread the love  WANANDOA na watu waliko kwenye mahusiano ya kimapenzi, wamekumbushwa...

Habari Mchanganyiko

Majaliwa: Mvua zimesababisha vifo vya watu 155, kuendelea hadi Mei

Spread the love  WAZIRI Mkuu, Kassim Majaliwa amesema mvua kubwa za El-Nino...

Habari Mchanganyiko

Exim Bank yatoa  vitanda kwa shule ya Jeshi la Polisi Moshi

Spread the love  BENKI ya Exim imekabidhii  seti ya vitanda kwa Shule...

error: Content is protected !!