Friday , 29 March 2024
Home Kitengo Habari Kimataifa Urusi yataja idadi ya wanajeshi wake waliofariki, yatofautiana na Ukraine
Kimataifa

Urusi yataja idadi ya wanajeshi wake waliofariki, yatofautiana na Ukraine

Spread the love

KWA mara ya kwanza Urusi imetangaza vifo vya wanajeshi wake 498 na wengine 1,597 kujeruhiwa tangu kuanza kwa vita kati yake na Ukraine. Anaripoti Mwandishi Wetu… (endelea)

Idadi hiyo inatofautiana kwa mbali na ile iliyotolewa na Jeshi la Ukraine ambapo lilidai wanajeshi 5, 840 wa Urusi wameuawa katika vita hiyo hadi sasa.

Pia Idara ya Usalama ya Uingereza katika taarifa yake ya kile kinachoendelea nchini Ukraine, imeonesha mashaka dhidi ya idadi iliyotolewa na Urusi.

Uingereza imedai kwamba Wizara ya Ulinzi ya Urusi imelazimishwa kutaja idadi hiyo ndogo na kwamba kuna uwezekano madhara ni makubwa zaidi kwa jeshi hilo.

MILIPUKO ZAIDI KYIV

Wakati hayo yakijiri, milipuko zaidi imeripotiwa katikati ya mji mkuu wa Ukraine, Kyiv na video katika mitandao ya kijamii zinaonesha milipuko mikubwa ya rangi ya machungwa angani.

Takribani milipuko minne imeripotiwa usiku wa kuamkia leo Alhamisi Machi 3, 2022.

Katika hatua nyingine jeshi la Ukraine limesema bado jiji la Mariupol lipo mikononi mwao na kwamba jeshi la Urusi halijafanikiwa kulitwaa.

Mji huo umeshuhudia mashambulizi mengi kutoka Urusi na unaonekana kuwa muhimu kwao kwani utawasaidia kuiunganisha na Ukreini upande wa kusini na mashariki.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoKimataifa

Zuma akataliwa kugombea urais

Spread the loveTUME Huru ya Uchaguzi Afrika Kusini (IEC) imemwondoa rais wa...

KimataifaTangulizi

Zuma akataliwa kugombea urais

Spread the love  TUME Huru ya Uchaguzi Afrika Kusini (IEC) imemwondoa rais...

Habari za SiasaKimataifa

Mwanaye rais jela miaka miaka 6 kwa dawa za kulevya

Spread the loveMwanawe rais wa zamani wa Guinea-Bissau amehukumiwa kifungo cha miaka...

Habari za SiasaKimataifa

Faye aahidi kuongoza kwa unyenyekevu, wagombea wenzie wakubali yaishe

Spread the loveMgombea wa upinzani Senegal, Bassirou Diomaye Faye anajiandaa kuwa rais...

error: Content is protected !!