April 17, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Meya Jacob kumng’oa Kubenea Ubungo?

Spread the love

KAULI ya Boniface Jacob, Diwani wa Kata ya Ubungo (Chadema) na Meya wa Manispaa ya Ubungo, kwamba hatogombea tena udiwani katika Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 2020, inaleta taswira mpya. Anaripoti Faki Sosi, Dar es Slaam…(endelea).

Kupitia ukurasa wake wa twitter leo tarehe 6 Aprili 2020, Jacob ameandika “Nimetangaza kung’atuka katika udiwani Kata ya Ubungo, muda wa madiwani utakapoisha. Sitogombea tena udiwani uchaguzi ujao..!

“Miaka 10 utumishi wangu ni kwa sababu wana-Ubungo mlinikopesha imani. Tumekuwa wote wakati wa shida na raha, mabonde na milima.”

https://twitter.com/MayorUbungo/status/1247055839447351297

Kwenye ujumbe wake huo, Jacob hajasema atagombea nafasi gani, lakini amekieleza chombo kimoja cha habari, kwamba anasubiri iwapo chama chake kitampa ridhaa ya kugombea ubunge katika Jimbo la Ubungo. Jimbo hilo kwa sasa linaongozwa na Saed Kubenea (Chadema).

error: Content is protected !!