April 13, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Chui aambukizwa corona

Spread the love

SHIRIKA la Habari la Uingrereza (BBC), limetengaza mnyama wa kwanza (Chui) kukutwa na virusi vya corona (COVID-19). Inaripoti Mitandao ya Kimataifa…(endelea).

Chui huyo wa kike anayetambulika kwa jina la Nadia (4), alikutwa katika bustani ya wanyama nchini Marekani, amepatikana na virusi vya corona.

Amepatikana akiwa kwenye Bustani ya Bronx katika Mji wa New York, inasema kwamba matokeo hayo yalithibitishwa na maabara ya huduma ya afya ya mifugo mjini Iowa.

”Nadia, na dadake Azul pamoja na Chui wengine wawili na simba watano wa Afrika, walianza kikohozi kikavu na wote wanatarajiwa kupona kabisa,” imesema taarifa ya uongozi wa bustani hiyo.

Chui hao wanaaminika kuambukizwa na mfanyakazi mmoja wa bustani hiyo.

”Tulimpima chui huyo kwa jina Nadia katika harakati za kuchukua tahadhari na tutahakikisha kwamba, maarifa yoyote tutakayopata kuhusu Covid-19 tutayasambazia ulimwengu unaojaribu kuelewa ugonjwa huu,” ilieleza taarifa hiyo ya jana Jumapili.

Hata hivyo wanyama wengine wanne katika bustani hiyo ikiwemo Chui na duma hawajaonyesha dalili zozote za ugonjwa huo.

”Wanyama wetu waliathiriwa na mtu ambaye alikuwa akiwaangalia, ambaye aliambukizwa virusi hivyo kabla ya kuanza kuonesha dalili,” imesema taarifa hiyo.

error: Content is protected !!