April 13, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Ireland yaahidi kuendeleza mapambano ya unyanyasaji

Spread the love

SERIKALI ya Irelanda imeahidi kuendelea na kupambana na vitendo vya ukatili wa kijinsia kwa wanawake na watoto nchini ili kutokomeza vitendo hivyo vinavyo changia kurudisha nyuma shughuli za maendeleo. Anaripoti Moses Mseti, Mwanza … (endelea).

Amesema wao wataendelea kuunga jitihada za serikali za kupambana na vitendo vya ukatili na kutokomeza mimba za utotoni pamoja na ndoa za utotoni ili kuongeza kasi ya maendeleo.

Kauli hiyo aliitoa jana na Naibu Mkuu wa Shirika la Maendeleo ya Ireland, Adrian Fitzgerald wakati hitimisho la siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia uliofanyika katika kijiji cha Mwawile kata ya Nhundulu wilayani Misungwi mkoani Mwanza.

Fitzgerald alisema wataendelea kuunga mkono wilaya ya Misungwi katika nyanja ya afya pamoja na kupambana na vitendo vya ukatili wa kijinsia ili kuhakikisha wanawake na watoto kukomesha vitendo hivyo.

“Tunataka familia zenye afya hapa misungwi na hatutaki kuona wanawake na wasichana wanakufa kutokana na kujifungua, tunataka kuondoa vifo vinavyotokea wakati wa kujifungua.

“Pia lazima sisi hapa tuhakikishe tunawapeleka watoto wetu wa kike shule ili tuweze kuwa na wanawake wenye uwezo wa kutunza familia zao na hiyo iende sambamba na kuondoa vipigo kwenye famili zetu,” alisema Fitzgerald.

Hata hivyo, aliwahimiza wazazi na walezi wote nchini kuhakikisha wanaacha vitendo vya kuwaozesha watoto kike ambao bado hawajafikisha umri wa miaka 18.

Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Kutetea Haki za Wanawake na Watoto (Kivulini) mkoani Mwanza, Yassin Ally, alisema kazi ya kupambana na vitendo vya ukatili inafanywa na makundi mengi ikiwemo jeshi la akiba (Sungusungu) katika vijiji na vitongoji vya wilaya ya Misungwi na kote nchini.

Mary Mpuya ni miongoni mwa wanawake waliofanyiwa vitendo vya ukatili na mume wake Jackson Maliki, alisema mumewe huyo kwa miaka mingi amekuwa akimfanyia vitendo vya ukatili ikiwemo kumchapa na kumfukuza nyumbani.

Alisema baada ya shirika la kivulini kufika kijijini kwao, mume wake alikwenda kusikiliza elimu iliyokuwa ikitolewa kuhusu wanaume kuacha kunyanyasa wanawake ambapo tangu siku hiyo (2018) alibadilika na kuanza kufanya shughuli za maendeleo nyumbani kwao.

error: Content is protected !!