Friday , 26 April 2024
Home Kitengo Maisha Afya IMF yaiahidi neema Tanzania
AfyaHabari Mchanganyiko

IMF yaiahidi neema Tanzania

Spread the love

 

RAIS wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, amefanya mazungumzo na Mkurugenzi wa Idara ya Afrika, Abebe Aemro Selassie kutoka Shirika la Fedha Duniani (IMF). Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Mazungumzo hayo, kuhusu masuala mbalimbali ikiwa ni pamoja na jinsi Shirika hilo litakavyosaidia Tanzania kukabiliana na ugonjwa wa Corona, yamefanyika leo Jumanne, tarehe 29 Juni 2021, Ikulu jijini Dodoma.

Rais Samia amekutana na mkurugenzi huyo ambaye aliambatana na ujumbe wake Ikulu Jijini Dodoma.

Selassie ametoa salamu kutoka kwa Mkurugenzi wa IMF, Kristalina Georgieva ambaye amemuhakikishia Rais Samia kuwa Shirika hilo litaendelea kushirikiana na Tanzania katika kufikia maendeleo yanayokusudiwa.

Akizungumzia kuhusu kukabiliana na ugonjwa Corona (Covid 19), amesema IMF ipo tayari kuendelea kufanyakazi na wataalam wa Tanzania kuandaa andiko litakalowezesha kupata msaada wa fedha kwa ajili ya kupambana na athari zitokanazo na ugonjwa wa Corona.

Pia, Selassie amesema, IMF itasaidia Tanzania kupata fedha kwa ajili ya kuimarisha sekta zilizoathirika na ugonjwa wa Corona ikiwa ni pamoja na sekta ya Utalii, Maji na Afya.

Kwa upande wake, Rais Samia amesema kupitia Kamati Maalum aliyoiunda kukabiliana na ugonjwa wa Corona, itashirikiana na wizara ya fedha kuandaa mpango wa jinsi ya kutekeleza maazimio ya ripoti maalum kwa ajili ya kukabiliana na ugonjwa huo wa Corona.

Rais Samia ameishukuru IMF kwa kuendelea kufanya kazi na Serikali yake kwa lengo la kuhakikisha Tanzania inapiga hatua kubwa ya kimaendeleo.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Afya

Mloganzila yajipanga kupandikizaji wa ini

Spread the love  HOSPITALI ya Taifa Muhimbili-Mloganzila imesema kutokana na uwekezaji uliofanywa...

Habari Mchanganyiko

Wakili: Ukimpa zawadi mwenza marufuku kumpora hata mkiachana

Spread the love  WANANDOA na watu waliko kwenye mahusiano ya kimapenzi, wamekumbushwa...

Habari Mchanganyiko

Majaliwa: Mvua zimesababisha vifo vya watu 155, kuendelea hadi Mei

Spread the love  WAZIRI Mkuu, Kassim Majaliwa amesema mvua kubwa za El-Nino...

Habari Mchanganyiko

Exim Bank yatoa  vitanda kwa shule ya Jeshi la Polisi Moshi

Spread the love  BENKI ya Exim imekabidhii  seti ya vitanda kwa Shule...

error: Content is protected !!