May 29, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Karia asalia peke yake uchaguzi TFF

Walace Karia, Rais wa TFF

Spread the love

 

KAMATI ya Uchaguzi ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania, (TFF), imepitisha jina la Wallace Karia kuwa mgombea peke kwenye uchaguzi mkuu wa Shirikisho hilo, huku wawili wakienguliwa. Anaripoti Kelvin Mwaipungu…(endelea)

Uchaguzi huo mwaka huu utafanyika Jijini Tanga tarehe 8 Agosti, huku uongozi uliopo sasa chini ya Wallace Karia ukimaliza muda wake katika kipindi cha miaka minne.

Wagombea hao wote watatu walifika mbele ya kamati hiyo, kwa nyakati tofauti kuanzia tarehe 25-27, kama ilivyoelezwa kwenye kalenda ya uchaguzi ya Shirikisho hilo.

Makamu Mwenyekiti wa kamati ya uchaguzi Wakili Benjamin Kalume amesema kuwa, wagombea hao wawili ambao ni Evans Mgeusa na Hawa Mninga, wameondolewa mara baada ya kukosa sifa ya uzoefu kwenye mpira wa Miguu kama ilivyoahinishwa kwenye kanuni namba 9, kanuni ndogo ya tatu.

“Kamati imewaengua wawili akiwemo Hawa Mninga na Evans Mgeusa na aliyepitisha ni Wallace Karia, kwa kuwa wawili hao kamati imeona wamekosa uzoezi, mara baada ya kupitia nyaraka zao.” Alisema Wakili Kalume

Kwa upande wa Wallace karia, makamu huyo Mwenyekiti wa kamati hiyo alisema kuwa, mgombea huyo aliweza kukizi vigezo vyote na kupitishwa kwa hatua inayofuata, “Karia aliweza kukizi vigezo vyote vilivyoahinishwa kwenye kanuni hivyo kamati imeona anapita kwa hatua inayofuata.”

Watatu hao walipitishwa na kamati hiyo kwenye mchujo wa kwanza, kati ya wagombea sita, waliofanikiwa kuchukua na kurejesha fomu.

Walioenguliwa kwenye hatua ya awali hapo awali na kamati hiyo mara baada ya kukosa wadhamini (Indorsement) ni Ally Saleh ‘Alberto’, Ally Mayay na Oscar Oscar.

error: Content is protected !!