Tuesday , 5 December 2023
Home Gazeti Habari za Siasa IGP Sirro: Namsubuiri Lissu
Habari za Siasa

IGP Sirro: Namsubuiri Lissu

Simon Sirro, Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini (IGP)
Spread the love

MKUU wa Jeshi la Polisi nchini (IGP), Simon Sirro amemweka kiporo Tundu Lissu, na kwamba anamsubiri atokeo alipo ili kutoa ushahidi wa kupigwa kwake risasi. Anaripoti Regina Mkonde … (endelea).

IGP Sirro ametoa kauli hiyo leo tarehe 18 Novemba 2019, wakati akihojiwa katika kipindi cha Konani kinachorushwa na Televisheni ya Mtandao ya ITV.

Amesema, upelelezi wa tukio hilo lililotokea mwaka 2017, umekwama kutokana na kukosekana kwa maelezo kutoka kwa Lissu, aliyekuwa Mbunge wa Singida Mashariki pamoja na dereva wake.

“Tumekosa ushirikiano, yeye mtendewa na shahidi wake hatujapata maelezo yao. Ndio maana tumesema Mungu amemsaidia afya yake imetengemaa, na anasema atakuja tutachukua ushahidi wake.

“Na yeye yupo si tunamsubiri tu aje, maana yake dereva tumetafuta hatukumpata, na bahati nzuri kesi ya jinai haifi, kesi ipo tunategemea Lissu aje,” amesema IGP Sirro.

Ni mwaka wa pili sasa Lissu, Mwansheria Mkuu wa Chadema yupo Ubelgiji. Ni baada ya kushambuliwa kwa risasi 16 zilizoingia mwilini mwake tarehe 7 Septemba 2017, nyumbani kwake ‘Area D’ jijini Dodoma muda mfupi baada ya kutoka kwenye shughuli za Bunge.

Pamoja na kumaliza matibabu, Lissu amesema, hawezi kurudi mpaka kutokana na vitisho vinavyotolewa vya kukatiza uai wake, ameitaka serikali imuhakikishie usalama wake.

Alitoa kauli hiyo katika mahojiano yake na kituo televisheni cha Sauti ya Marekani (VOA), ambapo alisisitiza kuwa hawezi kurudi Tanzania kwa kuwa bado kuna tishio la kuangamiza maisha yake.

“Nimebadili msimamo wangu wa kurejea Tanzania mwishoni mwa mwaka huu. Hii ni kwa sababu, bado naamini kuwa mazingira ya kiusalama kwangu, bado sio mazuri. Kuna watu kule nchini, wanaendelea kutoa vitisho kuwa wataangamiza maisha yangu,” ameeleza Lissu.

Anasema, “kuna watu wanaandika hadi kwenye mitandao ya kijamii. Kwamba ngoja aje, mara hii hatutakosea shabaha. Lakini serikali yangu imeshindwa kuchukua hatua.”

IGP Sirro akizungumzia tukio la Nape Nnauye, Mbunge wa Mtama kutishiwa bastola na mtu aliyemwita ‘asiyejulikana’ amesema, mhusika (Nape) hana maslahi na tukio hilo, na hivyo Jeshi la Polisi haliwezi kushughulikia suala hilo.

“Lile tukio bahati nzuri wote tuliliona, na bahati mbaya sidhani kama lilikuja polisi kutolewa taarifa, inaonekana mheshimiwa hakuwa na maslahi na ile kesi.

“Na kama alifungua, sikumbuki sawa sawa. Sitaki kumsemea. Wewe uliyefanyiwa ukaonekana huna maslahi, na ile kesi kama hujaonesha maslahi, sisi tunafanyaje? Kesi ni ya watu wawili,” amesema IGP Sirro.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Dk. Biteko: Viongozi tuache alama nzuri katika utendaji wetu

Spread the loveNaibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto Biteko...

Habari za SiasaTangulizi

Chanzo maporomoko yaliyoua 65 Hanang, chatajwa

Spread the loveSERIKALI imesema kumeguka kwa sehemu ya Mlima Hanang ambao ilikuwa...

Habari za Siasa

Baba yake Ole Sabaya ashinda Uenyekiti CCM – Arusha

Spread the loveLoy Thomas Sabaya ambaye ni Baba wa aliyekuwa Mkuu wa...

Habari za Siasa

Serikali yaagiza uchunguzi chanzo maporomoko Hanang

Spread the loveSERIKALI imeagiza uchunguzi ufanyike ili kubaini chanzo cha maporomoko ya...

error: Content is protected !!