October 2, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Waitara aagiza wanafunzi kupanda miti Mil 12

Spread the love

MWITA Waitara, Naibu Waziri wa Nchi – Ofisi ya Rais Tawala za mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), ameagiza wanafunzi milioni 12 wa Shule za Msingi na Sekondari nchini, kila mmoja kuhakikisha anapanda mti mmoja nyumbani kwao. Anaripoti Christina Haule … (endelea). 

Pia, mwanafunzi huyo ameagizwa kuhakikisha mti alioupanda, anauhudumia hadi ustawi ili kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi. 

Waitara ametoa kauli hiyo leo tarehe 18 Novemba 2019, kwenye Maadhimisho ya Siku ya Ugawaji wa Bendera ya Kijani katika programu ya mradi wa kuwaimarisha wanafunzi, kujifunza kuhifadhi mazingira uitwayo (Eco-schools).

Programu hiyo inaendeshwa na Shirika la kuhifadhi misitu ya asili Tanzania (TFCG), imefanyika katika Shule ya Msingi Lusanga, Mvomero mkoani humo.

“Nawaagiza, maofisa elimu wilaya, mikoa na wakurugenzi kusimamia, hakikisheni kila mwanafunzi anapanda mti na unakua” alisema Waitara.

Amesema, ufundishaji wa elimu ya utunzaji mazingira utasaidia kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi, na kuwa propramu ya TFCG imeenda sambamba na mipango ya Bunge ambalo hivi karibuni, limepitisha itifaki ili kuweza kukabiliana na mabadiliko hayo.

“Elimu inayotolewa na Echo Schools inamsaidia mtoto kufikiri na kupata jibu alilojifunza darasani, na kuepusha kupata watoto waliofaulu baada ya kufanya mchezo wa anadoo kwenye maswali ya kuchagua na kukosa wanaofaulu vzr baadaye,” amesema.

Charles Meshack, Mkurugenzi Mtendaji wa TFCG amesema, Echo schools ni programu inayotekelezwa nchi 67 ikiwa ni ya kimataifa iliyoasisiwa na Taasisi ya Elimu ya Mazingira Duniani mwaka 1994.

error: Content is protected !!