Tuesday , 5 December 2023
Home Gazeti Habari za Siasa Mchungaji Msigwa ajisalimisha Oysterbay
Habari za Siasa

Mchungaji Msigwa ajisalimisha Oysterbay

Mch. Peter Msigwa, Mbunge wa Iringa Mjini
Spread the love

MCHUNGAJI Peter Msigwa, Mbunge wa Iringa Mjini yuko njiani kujisalimisha katika Kituo cha Polisi cha Oysterbay, jijini Dar es Salaam. Ni baada ya mahakama kuagiza akamatwe. Anaripoti Regina Mkonde … (endelea).                

Msigwa ametoa taarifa hiyo leo tarehe 18 Novemba 2019, kupitia ukurasa wake wa Twitter, siku tatu baada ya Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kuagiza wabunge wanne wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kukamatwa, kwa kushindwa kufika mahakamani hapo.    

Mbunge huyo wa Iringa Mjini amesema, amepigiwa simu na Jeshi la Polisi, kumtaarifu kwamba anatakiwa kuripoti katika Kituo cha Polisi cha Oysterbay.

“Nimepigiwa simu na Jeshi la Polisi, natakiwa kuripoti kituo cha polisi cha Oysterbay Dar, niko njiani kuelekea huko,” ameandika Msigwa.

Msigwa anakuwa mbunge wa pili wa Chadema kujisalimisha kituoni hapo, baada ya Halima Mdee, Mbunge wa Kawe, kujisalimisha kituoni hapo siku ya Jumamosi iliyopita.

Wabunge wengine wanaotakiwa kujisalimisha polisi kwa amri ya mahakama ni Ester Bulaya (Bunda Mjini) na John Heche (Mbunge wa Tarime Mijijini).

Umuzi wa kukamatwa wabunge hao ulitolewa leo tarehe 15 Novemba 2019 na Hakimu Mkuu Mkazi wa mahakama hiyo, Thomas Simba kutokana na wabunge hao kushindwa kufika mahakamani.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Dk. Biteko: Viongozi tuache alama nzuri katika utendaji wetu

Spread the loveNaibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto Biteko...

Habari za SiasaTangulizi

Chanzo maporomoko yaliyoua 65 Hanang, chatajwa

Spread the loveSERIKALI imesema kumeguka kwa sehemu ya Mlima Hanang ambao ilikuwa...

Habari za Siasa

Baba yake Ole Sabaya ashinda Uenyekiti CCM – Arusha

Spread the loveLoy Thomas Sabaya ambaye ni Baba wa aliyekuwa Mkuu wa...

Habari za Siasa

Serikali yaagiza uchunguzi chanzo maporomoko Hanang

Spread the loveSERIKALI imeagiza uchunguzi ufanyike ili kubaini chanzo cha maporomoko ya...

error: Content is protected !!