Friday , 3 May 2024
Home Habari Mchanganyiko Huduma za fedha za simu za mkononi zinaweza kukuza kiwango cha uchumi wa taifa
Habari Mchanganyiko

Huduma za fedha za simu za mkononi zinaweza kukuza kiwango cha uchumi wa taifa

Sitoyo Lopokoiyit, Mkurugenzi Mtendaji wa M-Pesa Afrika
Spread the love

UTAFITI mpya umeonesha kuwa matumizi fanisi ya huduma za fedha za simu za mkononi yana mchango wa moja kwa moja katika ukuaji wa Kiwango cha Uchumi (GDP) katika  masoko yanayokua. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea)

Utafiti huo uliofanywa na kampuni ya Vodafone Group, Vodacom Group, Safaricom na Mpango wa Maendeleo wa Umoja wa Mataifa (UNDP), huduma hizo husaidia kupunguza gharama za biashara, kupata mkopo wa kuwekeza na kuwasiliana na wateja ambao hawakuwa na uwezo wa kufikia huduma za fedha hapo awali.

Utafiti wa mfano wa takwimu za uchumi ambao ulichunguza nchi 49 barani Afrika, Asia na Amerika Kusini, ulibainisha kuwa nchi zilizokuwa na huduma fanisi za fedha za simu za mkononi zilikuwa na ukuaji wa Kiwango cha Uchumi kwa kila mtu kwa mwaka cha hadi asilimia 1 zaidi kuliko nchi ambako mifumo ya huduma hizo hazikuwa fanisi au zilikuwa hazijaanzishwa.

Kulingana na utafiti wa awali wa Benki ya Dunia (World Bank) kuhusu uhusiano kati ya ukuaji wa uchumi na kupungua kwa idadi ya watu wanaoishi katika umaskini, ukuaji huu wa Kiwango cha Uchumi (GDP) kwa kila mtu unamaanisha kuwa nchi zenye huduma fanisi za fedha za simu za mkononi zinaweza kupunguza umaskini kwa karibu asilimia 2.6.

Uchanganuzi huu ulifanywa kama sehemu ya kampeni ya makampuni ya Africa.Connected, mradi wa kuendeleza ukuaji endelevu kupitia ushirikiano na kusaidia kuondoa tofauti zinazozuia maendeleo katika sekta kuu za uchumi barani Africa.

Sitoyo Lopokoiyit, Afisa Mkuu Mtendaji wa M-Pesa Africa na Afisa Mkuu wa Huduma za Fedha katika kampuni ya Safaricom, amesema “Mifumo ya huduma za fedha za simu za mkononi kama vile M-Pesa ni viendeshaji muhimu vya usawa wa kufikia huduma za fedha katika jamii, hali ambayo inaweza kuboresha fursa za maisha ya mtu binafsi na kuwezesha biashara kuanzishwa na kupanuka, na kuleta utajiri na ajira katika uchumi unaokua.”

“Ingawa bado kuna vizuizi vya kufikia mifumo hii ikijumuisha ufahamu wa masuala ya dijitali na ufikiaji wa simu mahiri na kuikuza na kiwango cha udhibiti usio sawa kwa watoa huduma za kisasa za fedha katika nchi nyingi,” amesema.

Ulrika Modeer, Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa na Mkurugenzi wa Ofisi ya Mahusiano ya Nje na Utetezi  katika shirika la UNDP, alisema, “Usawa wa ufikiaji wa huduma za fedha ni masharti ya mapema na kiwezeshaji muhimu cha kutimiza Malengo mengi ya Ukuaji Endelevu ya Umoja wa Mataifa (UN’s Sustainable Development Goals), ikijumuisha kupunguza umaskini, kukuza ukuaji wa uchumi, kuendeleza ufikiaji wa soko na kuhimiza uwekezaji katika sekta muhimu kama vile elimu, kilimo na afya.

Lakini muhimu zaidi, ni kuhusu kuwapa watu kipaumbele, kuwapa nguvu zaidi ya kudhibiti pesa zao na kukuza ukakamavu wao. Kuondoa hali za kutengwa kifedha barani Afrika, na duniani, lazima kiwe kipaumbele ikiwa tunatarajia kutimiza lengo la ustawi endelevu wa pamoja kwa ajili ya kila mtu katika dunia bora.”

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoTangulizi

Kimbunga “HIDAYA” chaendelea kuimarika, wananchi wapewa tahadhari

Spread the loveMAMLAKA ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) inaendelea kutoa taarifa...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Chadema waendelea kulilia katiba mpya

Spread the loveCHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimeendelea kudai upatikanaji wa...

BiasharaHabari Mchanganyiko

NMB yang’ara maonesho OSHA

Spread the loveBenki ya NMB imebeba tuzo ya kampuni bora kwenye sekta...

Habari MchanganyikoKimataifa

Ruto amteua Kahariri kuwa mkuu wa majeshi

Spread the loveRAIS wa Kenya, William Ruto, amemteua Jenerali Charles Muriu Kahariri,...

error: Content is protected !!