Saturday , 4 May 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Hoja ya Moshi kuwa Jiji yaibuliwa tena bungeni
Habari za Siasa

Hoja ya Moshi kuwa Jiji yaibuliwa tena bungeni

Spread the love

 

MBUNGE wa Moshi Mjini, Priscus Tarimo, ameitaka Serikali kupandisha hadhi ya utawala miji iliyokidhi vigezo, pamoja na kugawa mikoa yenye ukubwa wa kijiografia. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dodoma … (endelea).

Akizungumza katika kipindi cha maswali ya papo kwa papo kwa Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, leo Alhamisi, bungeni jijini Dodoma, Tarimo ameihoji Serikali kwa nini isipandishe hadhi halmashauri zilizokidhi vigezo vya kuwa jiji ikiwemo Halmashauri ya Wilaya ya Moshi.

“Nini mpango wa Serikali kugawa au kuongeza na kupandisha hadhi maeneo ya kiutawala ambayo yamekidhi vigezo? Kugawa, kuongeza au kupandisha hadhi maeneo ya kiutawala ambayo yamekidhi vigezo? Mfano kugawa mikoa mikubwa kama Tanga na Morogoro au kupandisha hadhi halmashauri kuwa majiji kama Halmashauri ya Manispaa Moshi?” amehoji Tarimo.

Spika wa Bunge, Dk. Tulia Ackson, alimtaka Waziri Majaliwa asilijibu swali hilo akisema ni mahususi kujibiwa na mawaziri wa kisekta.

“Hili manispaa ya Moshi nadhani yenyewe liko mahususi linahitaji lijibiwe na mawaziri wa kisekta,” amesema Spika Tulia.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaTangulizi

Sabaya afutiwa kesi, ruksa kugombea uongozi

Spread the loveMwendesha Mashtaka Mkuu wa Serikali DPP leo Ijumaa amefuta rufaa...

Habari za Siasa

Serikali yasaka bilioni 3 kujenga daraja Mto Mpiji

Spread the loveSerikali imesema inaendelea na juhudi za kutafuta fedha kiasi cha...

Habari za SiasaTangulizi

Chadema kwafukuta kisa chaguzi, Lissu aibua tuhuma nzito

Spread the loveCHAGUZI za kusaka viongozi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Chadema waendelea kulilia katiba mpya

Spread the loveCHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimeendelea kudai upatikanaji wa...

error: Content is protected !!