Friday , 26 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Hawa hapa wabunge Afrika Mashariki, Spika Tulia awapa maagizo
Habari za SiasaTangulizi

Hawa hapa wabunge Afrika Mashariki, Spika Tulia awapa maagizo

Angela Kizigha
Spread the love

SPIKA wa Bunge la Tanzania, Dk. Tulia Ackson, amewataka wabunge tisa wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EALA), kusimamia maslahi ya Tanzania pamoja na kuwasilisha hoja za nchi badala ya hoja zao binafsi. Anaripoti Regina Mkonde, Dar es Salaam…(endelea).

Spika Tulia ametoa agizo hilo leo Alhamisi, tarehe 22 Septemba 2022, bungeni jijini Dodoma, muda mfupi baada ya Katibu wa Bunge, Nenelwa Mwihambi, kuwatangaza washindi wa uchaguzi wa EALA.

“Wabunge hawa ndiyo wabunge tumewachagua sisi siku ya leo kwa niaba ya wananchi wote kwenda kutuwakilisha kama Tanzania kwenye Bunge la Afrika Mashariki na tunawategemea mnapokwenda kule si hoja ya mawazo yenu, ni hoja ya nchi inasemaje na tunaamini mtaenda kusimamia maslahi ya nchi kama mlivyoahidi hapa,” amesema Spika Tulia.

Dk. Ng’waru Maghembe

Aidha, Spika Tulia amewataka wabunge hao wateule kuzingatia majukumu yao watakayopewa na EALA, pamoja na kutoa mrejesho kwa Bunge la Tanzania juu ya kazi watakazozifanya.

Dk. Abdula Hasnuu Makame,

“Niwape ushauri kama ambavyo sisi huwa tunaenda majimboni kwetu, ninyi jimbo lenu ni hili hapa kwa niaba ya Watanzania. Lakini muhimu kuzingatia kazi zile ambazo mnapaswa kuzifanya huko, huku lazima mtupatie taarifa kwa kazi zenu kwa kadiri ambayo mnatakiwa kufanya hivyo na kanuni,” amesema Spika Tulia.

Wabunge hao wateule ni Angella Kiziga, aliyepata kura 322, zilizopigwa katika kundi  la wagombea wanawake, mwingine katika kundi hilo ni Nadra Juma Mohammed (310), Dk. Shogo Mlozi (322).

Wabunge waliochaguliwa kutoka kundi la wagombea kutoka Zanzibar, ni Abdullah Makame aliyepata kura 305, kati ya kura 311 zilizopigwa na Machano Ally Machano (291).

Mashaka Ngole, kutoka Chama cha Wananchi (CUF), amechaguliwa katika kundi la wagombea wa vyama vya waliowachache bungeni, ambapo amepata kura 234, kati ya kura 319 zilizopigwa.

Angela Kizigha

Kwa upande wa kundi la wagombea wa Tanzania Bara, walioshinda ni Ansar Abubakar Kachwamba, aliyepata kura 300 kati ya kura 313 zilizopigwa. Wengine ni James Kinyasi Millya (312) na Dk. Ngwalu Jumanne Maghembe (311).

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Prof. Muhongo akomalia matumizi nishati jadidifu kuondoa uhaba wa umeme

Spread the love  MBUNGE wa Musoma Vijijini (CCM), Profesa Sospeter Muhongo, ameendelea...

Habari za Siasa

Kilosa yawa mfano wa kuigwa miradi ya Mwenge nchini

Spread the love  KIONGOZI wa Mbio za Mwenge Kitaifa Godfrey Mzava amezitaka...

Habari za SiasaTangulizi

Biteko ataja vipaumbele 7 bajeti nishati 2024/25

Spread the love  NAIBU Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Mwekezaji amwaga bil. 39 kujenga viwanda 3 vya uchenjuaji

Spread the loveKampuni ya Mineral Access System Limited (MAST) inayoiwakilishwa kampuni ya...

error: Content is protected !!