Tuesday , 23 April 2024
Home Habari Mchanganyiko Wavunaji mkaa watakiwa kufuata sheria, kanuni na taratibu
Habari Mchanganyiko

Wavunaji mkaa watakiwa kufuata sheria, kanuni na taratibu

Mary Masanja
Spread the love

SERIKALI imewataka wananchi wanaofanya biashara ya mkaa kufuata sheria, kanuni na taratibu kwa kuwa kumekuwepo na wimbi la uvunaji wa mazao ya misitu, ukataji na uchomaji wa mkaa bila kufuata sheria zinazosimamia biashara hiyo. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea).

Hayo yamesemwa leo Septemba 22, 2022 na Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mary Masanja kwa niaba ya Waziri wa Maliasili na Utalii alipokuwa akijibu swali la Mbunge wa Mbogwe, Nicodemus Maganga (CCM).

“Inapotokea mwananchi anasafirisha mazao ya misitu (mkaa) bila kufuata utaratibu, mazao hayo hutaifishwa na Serikali” Masanja amesisitiza.

Amesema uvunaji holela wa mkaa umesababisha kutoweka kwa kasi kwa maeneo ya misitu na hatimaye kujitokeza kwa athari za mabadiliko ya tabia nchi.

Kuhusu kauli ya Serikali juu ya askari wa Misitu wanaopiga na kuwanyang’anya mkaa wananchi wa Mbogwe, Masanja amesema Wizara haitosita kuwachukulia hatua watumishi wake wanaohusika na uvunjaji huo wa sheria, kanuni na taratibu.

Pia, amewataka wananchi kutoa taarifa kwa vyombo vya ulinzi na usalama wanapotendewa vibaya na watumishi hão ili hatua stahiki zichukuliwe.

Akijibu swali la nyongeza la Mbunge wa Tabora Mjini, Emmanuel Mwakasaka aliyehoji lini Serikali itatoa vibali vya Uwindaji, amesema vibali vya uwindaji wa kitalii vinaendelea kutolewa kwa mujibu wa kanuni husika ambapo hadi sasa jumla ya minada saba imefanyika na wadau wamepewa vibali vyao.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Watuhumiwa 12 wa kilo 726.2 za dawa za kulevya wafikishwa mahakamani

Spread the love  WATUHUMIWA watatu wamefikishwa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kibaha Mkoani...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Mwekezaji amwaga bil. 39 kujenga viwanda 3 vya uchenjuaji

Spread the loveKampuni ya Mineral Access System Limited (MAST) inayoiwakilishwa kampuni ya...

Habari Mchanganyiko

GGML yasisitiza kuendelea kuimarisha afya za wafanyakazi

Spread the loveKAMPUNI ya Geita Gold Mining Limited kwa kushirikiana na kampuni...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

NMB yadhamini Mkutano Mkuu ALAT, kufunguliwa na Samia

Spread the loveBENKI ya NMB, imekabidhi hundi yenye thamani ya Sh. 120...

error: Content is protected !!