MRISHO Gambo, mgombea ubunge Jimbo la Arusha mjini kupitia Chama Cha Mapinduzi(CCM), ameamua kubadili mtindo wa kummaliza Godbless Lemba, mgombea ubunge wa jimbo hilo anayetetea nafasi yake kwenye uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika tarehe 28 Oktoba 2020. Anaripoti Mwandishi Wetu, Arusha … (endelea).
Amesema, tayari zimebaki kata tatu ili akamilishe kata zote za jimbo hilo alizofanya mikutano ya hadhara na kisha atabadili mtindo na kwenda nyumba kwa nyumba kusaka kura.
“Tumefanya mikutano zaidi ya kata 20, hizi tatu zilizobaki tukimaliza tunaanza kampeni za nyumba kwa nyumba, mlango kwa mlango na ikibidi kitanda kwa kitanda,” amesema Gambo wakati wa ufunguzi wa kampeni za Kata ya Sekei, jijini humo.
Amewataka wakazi wa kata hiyo kutofanya makosa na kwamba, wachagua wagombea wanaotokana na chama hicho katika ngazi zote kuanzia udiwani, ubunge na urais.

Awali, baada ya kupitishwa na chama chake kugombea ubunge kwenye jimbo hilo, Lema alisema kama sheria ingeruhusu, alitamaba kushindana na CCM wote kwenye jimbo hilo na angewashinda kwa kupata kura nyingi.
Yupo tayari kualiwaomba wakazi wa kata hiyo kukipigia kura CCM kwa mtindo wa mafiga matatu yaani diwani, mbunge na rais ili iwe rahisi kupenyeza hoja za vipaumbele vya jimbo lake.
Siasa Hadi majeshini?. IJP simaama kidete Askari wanajisahau Sana.