Tuesday , 30 May 2023
Home Gazeti Habari za Siasa Maalim Seif akwepa kitanzi cha NEC
Habari za SiasaTangulizi

Maalim Seif akwepa kitanzi cha NEC

Spread the love

MAALIM Seif Sharif Hamad, mgombea urais wa Zanzibar kupitia Chama cha ACT-Wazalendo, ameshindwa kumnadi kwa jina Tundu Lissu, mgombea urais wa Tanzania kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema). Anaripoti Mwandishi Wetu, Kigoma … (endelea).   

Akiwa kwenye mkutano wake wa hadhara katika eneo la Kibirizi, Jimbo la Kigoma Mjini mwishoni mwa waiki iliyopita, aliwataka wananchi wa jimbo hilo kumpigia kura mgombea wa upinzani anayekubalika na ambaye anaweza kumshinda Dk. John Magufuli, mgombea urais kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Ni mara ya kwanza Maalim Seif kumnadi mgombea wa upinzani bila kumtaja jina, ambapo awali akiwa visiwani Zanzibar, nguli huyo wa siasa za upinzani nchini aliwataka Watanzania kumchagua Lissu.

Tayari Lissu na Freeman Mbowe ambaye ni mwenyekiti wa Chadema Taifa, wamewatakwa Wazanzibari visiwani humo kumchagua Maalim Seif kwa kuwa, ndiye anayekubalika kwa watu wengi.

Hata hivyo, Msajili wa Vyama vya Siasa, ilieleza kwamba ‘kuungana’ kwa vyama kama ilivyokuwa ikinadiwa kati ya ACT-Wazalendo na Chadema, ni kinyume cha sheria kwa kuwa taratibu hazijafuatwa.

Tundu Lissu, Mgombea Urais Tanzania (Chadema).

Sisty Nyahoza ambaye ni Naibu Msajili alisema, iwapo vyama vya siasa vinataka kuungana, vinatakiwa kufuanya hivyo kabla ya miezi mitatu kuingia kwenye uchaguzi na taarifa ya muungano huo, inapaswa kuwasilishwa kwenye ofisi yake.

Akiwa Kibirizi, Maalim Seif bila kutaja jina Lissu kama alivyofanya visiwani Zanzibar, amesema  “sisi tumeshafanya uamuzi wa kuona mgombea gani anafaa kutuvusha kambi ya upinzani katika mchakato wa kumpata mgombea anayeweza kumshinda Rais Magufuli, ninyi wenyewe mnaona tunaomba mumuunge mkono kumpiga kura kiongozi huyo hata kama hatoki kwenye chama chetu.”

Akisisitiza msimamo huo, Maalim Seif amesema, kulingana na mazingira ya saisa za Tanzania yalivyo, bila wapinzani kuungana, itakuwa ni kazi kubwa kuing’oa CCM madarakani.

Pia Maalim Seif amewataka wakazi wa Jimbo la Kigoma Mjini kumchagua Zitto Kabwe, mgombea ubunge kwenye jimbo hilo kwa kuwa, ni mtumishi ndani na nje ya jimbo hilo.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaTangulizi

Uamuzi juu ya wakurugenzi kusimamia uchaguzi 13 Juni

Spread the love  MAHAKAMA ya Afrika ya Haki za Binadamu (ACHPR), imepanga...

Habari MchanganyikoTangulizi

Jeshi la Polisi kushirikiana na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam katika utafiti

Spread the love  JESHI la Polisi Nchini limesema kuwa katika kukabiliana na...

KimataifaTangulizi

Mtuhumiwa wa mauaji ya halaiki ya Rwanda akamatwa Afrika Kusini

Spread the love  MMOJA wa watuhumiwa wakuu wa mauaji ya Kimbari ya...

Habari za Siasa

Musoma Vijijini waomba ujenzi wa barabara uanze haraka

Spread the loveJIMBO la Musoma Vijijini, mkoani Mara, limeomba Serikali kuhakikisha ujenzi...

error: Content is protected !!