Saturday , 27 April 2024
Home Habari Mchanganyiko Flaviana Matata Foundation, Marie Stopes yaamsha ari matumizi ya taulo za kike kipindi cha hedhi
Habari Mchanganyiko

Flaviana Matata Foundation, Marie Stopes yaamsha ari matumizi ya taulo za kike kipindi cha hedhi

Spread the love

MWANAMITINDO maarufu nchini Tanzania, Flaviana Matata kwa kushirikiana na Taasisi MarieStopes Tanzania wameitaka jamii kuamini hedhi iwe kama moja ya maisha ya kawaida ya msichana na mwanamke ili kuondokana na vitendo vya unyanyapaa wanavyofanyiwa watoto wa kike pindi wanapokuwa katika hali hiyo. Anaripoti Mary Victor…(endelea).

Kwa mujibu wa Flaviana na Marie Stopes, Siku ya hedhi huadhimishwa kila tarehe 28 Mei 2022 kila mwaka ina lengo la kuwakutanisha wadau mbalimbali kwa dhumuni la kuongeza uelewa kuhusu masuala ya hedhi kwa msichana na kuhamasisha msichana kupata maji safi na taulo hasa wale walio katika kipato duni.

Hii inamwezesha anapoingia katika siku za hedhi aweze kujistiri na kuendelea taratibu nyingine kama kuhudhiria masomo, shughuli mbalimbali za kijamii ikiwemo michezo na burudani.

Akizungumza katika maadhimisho hayo, Meneja mawasiliano wa Marie Stopes, Ester Shedafa alisema, “Marie Stopes kwa kushirikiana na Flaviana Matata Foundation tumetoa elimu ya masuala ya hedhi salama kwa wasichana na wavulana 987 katika shule ya Sekondari Bukandw, Wilaya ya Magu (Mwanza).

Pamoja na mambo mengine, Ester alisema baada ya mafunzo, mashirika hayo mawili (Marie Stopes na Flaviana Matata Foundation) walikabidhi zawadi mbalimbali kwa wanafunzi shuleni hapo ikiwemo taulo za kike kwa wasichana.

“Katika kuadhimisha siku hii ya hedhi, tunatoa wito kwa mashirika binafsi, walimu pamoja na serikali yetu sikivu kusisitiza utolewaji wa elimu ya masuala ya hedhi kwa vijana wa kike na kiume ili kuwawezesha kutambua mabadiliko ya mwili na kukabiliana nayo pamoja na kufahamu namna ya kujisitiri kipindi anachoingia katika hali hiyo.

“Kwa upande wa watoto wa kiume elimu hiyo imetolewa ili kuwajengea uelewa wa mabadiliko hayo kama mshiriki mwenza ili kuondoa unyanyapaa pale msichana anapokuwa katika hedhi,” alisema na kuongeza:

“Kwa upande wa mashirika ya maendeleona taasisi mbalimbali kuzisaidia jamii kwa namna mbalimbali kuhakikisha wasichana hasa walio shuleni wanakuwa na mazingira rafiki hasa katika shughuli za michezo ili wanapoingia kwenye hedhi wasikose mahitaji yao muhimu yatakayoweza kusababisha washindwe kushiriki shughuli za masomo, michezo pamoja na mambo mbalimbali.”

Kwa upande wake, Mwanamitindo Flaviana Matata alisema, “ni vyema kuangalia upya suala la bei za taulo za kike pamoja na upatikanaji wa maji  safi ili kusaidia maeneo yenye uhitaji kwa lengo la kuwasaidia wasichana waweze  kupata taulo za kujistiri kwa muda wa mwaka mzima ili waweze kuwa na mahudhurio mazuri shuleni.”

“Hedhi salama ni pamoja na mtoto wa kike kupata mahitaji yake yote muhimu akiwa kwenye siku zake za hedhi yakiwamo maji safi na salama na sehemu salama ya kubadilishia taulo hizo,” alisema

Alisema, “wataalamu wa afya wanasema kwamba mtoto wa kike akipata hedhi salama ataweza kuondokana changamoto nyingi za kiafya ikiwemo muwasho, fangasi, maumivu pamoja na hedhi bila kutokwa na damu nyingi na hivyo kuwa hedhi yenye amani na furaha.”

Mwanamitindo huyo alisema, “suala la hedhi halipaswi kuwa kero kwa mtoto wa kike, hata hivyo imekuwa tofauti kwa watoto wengi wa kike ambao wamekuwa wakipata wasiwasi na kukosa raha pindi wanapokaribia mzunguuko wao, hali hii inasababishwa na changamoto ambazo watoto wa kike wanazipata katika kupata hedhi salama.”

Alisema hedhi salama inachangia watoto wa kike kushiriki shughuli za kuinua pato la taifa hili ikiwemo shughuli za mitindo, michezo mbalimbali pamoja na kufaulu vyema masomo hayo. Suala la kusisitiza ni kwa jamii kuachana na mila potofu zinazorudisha nyuma harakati hizi za kumfanya mtoto wa kike aamini kwamba hedhi ni moja ya sehemu katika maisha yake.

Kwa mwaka huu maadhimisho hayo yamefanyika jijini Mwanza huku kauli ya serikali pamoja na mambomengine ikikisitiza; “Upatikanaji wa huduma na vifaa vya kujihifadhi hasa taulo za kike ziwepo sehemu zote kwa makundi yote kwa bei nafuu katika jamii”.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Wakili: Ukimpa zawadi mwenza marufuku kumpora hata mkiachana

Spread the love  WANANDOA na watu waliko kwenye mahusiano ya kimapenzi, wamekumbushwa...

Habari Mchanganyiko

Majaliwa: Mvua zimesababisha vifo vya watu 155, kuendelea hadi Mei

Spread the love  WAZIRI Mkuu, Kassim Majaliwa amesema mvua kubwa za El-Nino...

Habari Mchanganyiko

Exim Bank yatoa  vitanda kwa shule ya Jeshi la Polisi Moshi

Spread the love  BENKI ya Exim imekabidhii  seti ya vitanda kwa Shule...

Habari Mchanganyiko

NBC yakabidhi vitanda Shule ya Polisi Moshi

Spread the loveBenki ya NBC imekabidhi msaada wa vitanda 28 kwa Shule...

error: Content is protected !!