July 3, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Kiwanda cha Dawa Kairuki chapongezwa, SADC yatajwa

Spread the love

KAMATI Afya ya Bunge la Zambia imepongeza uwekezaji wa wazawa wa Kiwanda cha Kutengeneza Dawa cha Kairuki nchini Tanzania wakisema ni njia ya bora ya kukuza uchumi wa nchi na kupunguza gharama kubwa kuagiza nje ya nchi vifaatiba. Anaripoti Mwandishi Wetu, Kibaha…(endelea).

Hayo yalisemwa Ijumaa ya tarehe 27 Mei 2022 na Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Dk. Christopher Kalila alipoongoza ujumbe wa kamati yake kutembelea Kiwanda cha Kairuki Pharmaceutical LTD kilichopo Kibaha, Mkoa wa Pwani.

Dk. Kalila alisema ziara hiyo nchini ina lengo la kujifunza masuala mbalimbali ikiwemo uwekezaji unaofanywa na wazazi kwenye sekta ya afya hasa ikizingatiwa Tanzania na Zambia ni marafiki wa kipindi kirefu.

Alisema janga la UVIKO-19 linapaswa kuwa somo kwa nchi hususan za Afrika kuanza kutengeneza bidhaa zake wenyewe kwani mipaka na safari zilipozuiwa, kulisababisha baadhi ya huduma kukosekana au kupanda bei.

Mwenyekiti huyo alisema wameona jinsi kiwanda hicho kinavyoweza kupunguza gharama za kuagiza nje lakini kutumia soko la Nchi za Jumuiya ya Kusini mwa Afrika (SADC) kuuza bidhaa wanazozalisha.

Awali, Meneja wa Kiwanda hicho, Ellen Magita aliwapokea wageni hao na kufanya nao mazungumzo kisha kuwatembeleza maeneo mbalimbali ya kiwanda huku akisema ujio wa wabunge hao unaweza kuwanufaisha kwa kuweza kupeleka dawa nchini mwao.

Ellen alisema kiwanda hicho kilianza uzalishaji wa majitiba ‘dripu’ mwaka 2020 kikiwa kimechelewa kwa mwaka mmoja kutokana na changamoto mbalimbali hususan ugonjwa wa UVIKO-19.

Alisema kina uwezo wa kuzalisha chupa za majitiba milioni 55 kwa mwaka na mpaka sasa tayari wamepeleka zaidi ya chupa milioni moja katika Bohari ya Dawa.

“Kiwanda hiki kimesimwikwa kwa teknolojia ya hali ya juu ambayo kwa nchi zote za Afrika Mashariki na kati sisi ndio tunaongoza lakini pia inakubalika na Shirika la Afya Duniani hivyo bidhaa tunazozitoa zinakubalika kote,” alisema Ellen

Kuhusu uwekezaji wa kiwanda hicho cha mzawa, alisema kimetumia zaidi ya Sh.47 bilioni.

Meneja huyo alisema, mitakati ya kiwanda ni kuzalisha majitiba katika ujazo mdogo na ndani ya miezi 18 watapanua zaidi kuanzia ujazo wa Mills 2 mpaka 20.

Alisema wanatarajia kuanza kuzalisha vifaatiba mbalimbali vinavyotumika hospitalini na kutumia soko la nchi za SADC.

error: Content is protected !!