Sunday , 28 April 2024
Home Habari Mchanganyiko Exim yamwaga zawadi ya pesa, simu kwa washindi wa “Chanja Kijanja, Kimasta Zaidi’’
Habari Mchanganyiko

Exim yamwaga zawadi ya pesa, simu kwa washindi wa “Chanja Kijanja, Kimasta Zaidi’’

Spread the love

BENKI ya Exim Tanzania imeendelea kugawa zawadi mbalimbali ikiwemo fedha taslimu na simu janja (smartphones) kwa washindi wa kampeni yake  “Chanja Kijanja, Kimasta Zaidi’’ inayolenga kuhamasisha wateja wa benki ya Exim kutumia kadi zao za Mastercard katika manunuzi ya mtandaoni au kufanya malipo kupitia mashine za malipo (POS) katika maduka mbalimbali na maeneo mengine nchini. Anaripoti Mwandishi Wetu…(endelea).

Kampeni hiyo iliyozinduliwa mapema mwezi Novemba inatoa fursa kwa wateja wa benki hiyo wanaotumia kadi zao za Exim Mastercard kufanya miamala, kuwa kwenye nafasi ya kujishindia zawadi mbalimbali ikiwemo fedha taslimu, Simu janja (Smart Phones) na safari zilizolipiwa gharama zote kwenda mapumziko katika mataifa ya Dubai, Uturuki na Afrika Kusini wao pamoja na wenza wao.

Akizungumza kwenye hafla fupi ya kukabidhi zawadi hizo kwa washindi hao ikiwemo zawadi ya simu janja aina ya  Iphone 14 Pro kwa mshindi wa mwezi ambae ni Emanuel Lutambi mkazi wa mkoa wa Iringa, Afisa Idara ya Huduma Mbadala Kupitia Mifumo ya Kidigitali wa Benki ya Exim, Gregory Malembeka alisema hadi kufikia sasa zaidi ya washindi 100 wameshajishindia zawadi ya fedha kiasi cha Tsh 100,000 kila mmoja kupitia  droo “bahati nasibu” na mitandao.

Meneja wa Benki ya Exim tawi la Mkoa wa Iringa, Michael Richard (wa pili kushoto) sambamba na maofisa wengine wa benki hiyo Aziza Msangi (kushoto) na Bw. Emanuel Bayo (Kulia) wakikabidhi zawadi ya simu janja  aina ya  Iphone 14 Pro kwa Emanuel Lutambi mkazi wa mkoa huo baada ya kuibuka mshindi wa droo ya mwezi ya kampeni ya “Chanja Kijanja, Kimasta Zaidi’’ inayolenga kuhamasisha wateja wa benki hiyo kutumia kadi zao za Mastercard katika manunuzi ya mtandaoni au kufanya malipo kupitia mashine za malipo (POS).

“Inafahamika kwamba kipindi hiki cha kuelekea mwisho wa mwaka kinahusisha manunuzi zaidi kutokana na sherehe na sikukuu ya Christmas. Wito wetu kwa wateja wetu ni wao kufanya manunuzi kwa kutumia Exim Mastercard iwe mtandaoni au kwenye mashine za malipo (POS) ili waweze kujiweka kwenye nafasi ya kushinda kwa kuwa zawadi bado ni nyingi.’’

“Ifahamike kwamba unapochanja au kulipia bidhaa au huduma basi unajiweka kwenye nafasi ya kuingia kwenye droo ya kushinda safari zilizolipiwa kila kitu kikamilifu kwa siku tano kwenda Dubai, Uturuki au Afrika Kusini pamoja na mpendwa wako. Pia unaweza kuwa mshindi wa iPhone 14 pro inayotoka kila mwezi au pesa taslimu100,000 inayotoka kila wiki….ujanja ni kuchanja tu na Exim Mastercard,” alisema.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Mvungi aendesha kikao kazi cha wataalam wa Regrow

Spread the love  MKURUGENZI wa Idara Sera na Mipango Wizara ya Maliasili...

Habari MchanganyikoTangulizi

Jacob, Malisa waachiwa kwa masharti

Spread the love  JESHI la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam,...

Habari Mchanganyiko

Polisi wakanusha kufanya uzembe ajali iliyouwa mwandishi Ayo Tv

Spread the loveJESHI la Polisi limekanusha tuhuma zilizoibuliwa dhidi yake  kwamba limekawia...

Habari Mchanganyiko

Rais Samia kuzindua gazeti litakalotoa habari za wafanyakazi Tanzania

Spread the loveSHIRIKISHO la Vyama vya Wafanyakazi Tanzania (TUCTA), liko mbioni kufufua...

error: Content is protected !!