March 8, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Ester Bulaya atiwa nguvuni Tarime

Spread the love

ESTER Bulaya, Mbunge wa Bunda Mjini anashikiliwa na polisi wilayani Tarime kwa mahojiano, anaandika Hamisi Mguta.

Imeelezwa kuwa Bulaya amekamatwa kwa kosa la kuhutubia mkutano wa hadhara katika jimbo la Tarime, ambalo si jimbo lake jambo ambalo linakwenda kinyume na agizo la Rais.

Wabunge Esther Matiko na John Heche wameongozana naye kufika katika ofisi ya RCO.

Tumaini Makene, Afisa Habari wa Chadema ameiambia MwanaHALISI Online kuwa Bulaya amekamatwa na yuko kituo cha polisi Tarime Rorya kuhojiwa ni kwanini aliudhuria mkutano wa hadhara wa Mbunge wa Tarime vijijini uliofanyika jana nyamongo.

“Mikutano ya hadhara inafanyika kwa mujibu wa sheria na sheria haimzuii mtu yoyote kuhudhuria  mikutano ya kisiasa, kama mikutano yetu inaudhuriwa hadi na watu wa CCM, sembuse Ester Bulaya ambaye ni Mjumbe kwenye Kamati Kuu ya chama?,” alihoji Makene.

error: Content is protected !!