October 2, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Elimu Bure ina changamoto -Ripoti

Prof. Joyce Ndalichako, Waziri wa Elimu

Spread the love

WADAU wa elimu nchini, wameishauri serikali kupitia upya sera ya elimu bure, ili kuondoa changamoto zinazojitokeza katika utekelezaji wake. Anaripoti Regina Mkonde…(endelea).

Ushauri huo umetolea leo tarehe 11 Desemba 2019, katika hafla ya uzinduzi wa Ripoti ya Saba ya Tathimini ya Kiwango cha Kujifunza Tanzania, iliyofanyika jijini Dar es Salaam.

Miongoni mwa wadau walioshiriki kwenye uzinduzi huo, wameangazia changamoto ya uhaba wa walimu, miundombinu kama madarasa na maktaba pamoja na vitabu.

Profesa Eugine Kafanabo, Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM)amesema sera hiyo ni nzuri lakini inahitaji kupitiwa upya, ili kuhakikisha serikali inatenga bajeti ya kutosha, itakayowezesha kuboresha miundombinu ikiwemo madarasa na maktaba, pamoja kusadia upatikanaji wa vitabu.

Prof. Kafanabo ameshauri changamoto hizo zipatiwe ufumbuzi ili kuhakikisha wanafunzi wote wanapata haki sawa kwa bajeti ya kutosha.

“Sera ya elimu bila malipo ni nzuri ila tunatakiwa kufanya “review” , ili kuhakikisha wanafunzi wote wanapata haki sawa kwa bajeti ya kutosha. Tuhakikishe madarasa yanakuwepo, vitabu, maktaba na hata ikibidi chakula kitolewe ili kuiboresha elimu hii,”ameshauri Prof. Kafanabo.

Daktari Joeli Kayombo kutoka Chuo Kikuu Kishiriki cha Elimu Dar es Salaam (DUCE)amesema sera nyingi zinahamasisha watoto kwenda shule, lakini kuna pengo kubwa katika kuhakikisha watoto hao wanapata elimu stahiki, hasa kwa watoto wanaotaka kwenye kaya masikini.

“Sera nyingi zinahamasisha watoto waende shule, ila nini kinatokea wanapokuwa madarasani hapo ndipo tatizo linapoanza. Achivement gape” inaonekana kwa uwazi sana, kwa kaya masikini na zenye uwezo na hata katika matokeo hili linaonekan,” ameeleza Dk. Kayombo.

error: Content is protected !!