Saturday , 20 April 2024
Home Habari Mchanganyiko Mamia wamlilia Marehemu Ali Mufuruki
Habari Mchanganyiko

Mamia wamlilia Marehemu Ali Mufuruki

Spread the love

MAISHA ya mfanyabiashara bilionea, Ali Abdul Mufuruki (60), aliyefariki dunia Jumapili iliyopit, nchini Afrika Kusini, yamegusa watu wengi na kutoka kada tofauti.  Anaripoti Faki Sosi … (endelea).

Miongoni mwa walioguswa na maisha ya Mufuruki, ni pamoja na aliyekuwa Balozi wa Tanzania nchini Afrika Kusini, Ami Mpungwe.

Mwili wa Mufuruki uliagwa leo, katika  ukumbi wa mikutano wa kimataifa wa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere (JNICC), jijini Dar es Salaam.  

Baadhi ya watu mashuhuri waliohudhuria, ni pamoja na Rais mstaafu, Benjamin William Mkapa, Balozi Mpungwe; MkurugenziMtendaji wa Taasisi Binafsi Tanzania (TPSF), Godfrey Simbaye.

Akizungumza katika hafla ya kuaga mwili wake, Balozi Mpugwe alisema, “Mufuruki alikuwa mzalendo kwa vitendo.”

Alisema, “Mufuruki aliacha kazi nchini Ujerumani baada ya kumaliza masomo yake na kwa uzalendo wake, alikuja nchini mwake Tanzania kutafuta kibarua.”

Alisema, hekima, unyenyekevu, uwezo wa akili aliokuwa nao darasani, ndivyo vilivyomwezesha Mufuruki, kushiriki midahalo ya ndani na nje ya Tanzania, pamoja kuaminiwa na taasisi mbalimbali.

Naye Simbaye, akizungumza katika hafla hiyo, ameweka wazi matamanio yake ya kumtaka Mufuriki kuwa kuwa mwenyekiti wa taasisi hiyo, kuchukua mikoba ya Dk. Reginald Mengi, aliyefariki dunia Mei mwaka huu.

“Mufuruki amekuwa kwenye bodi nyingi, lakini kuna kitu hajakifanya na nilitamani akifanye. Nilitaka awe mwenyekiti wa TPSF, lakini Mwenyezi Mungu amemchukua kabla ya hilo kutimia,” alieleza Simbaye, huku akibubujikwa na machozi.

Simbaye aliyeonekana kuguswa na kifo hicho cha Mufuriki ameeleza maelfu ya waombelezaji kuwa Mufuruki ameacha pengo kubwa kwenye sekta ya biashara nchini.

Naye Magrath Ikongo, Kaimu Mwenyekiti wa Bodi ya kampuni ya simu za mikononi wa Vodacom Tanzania, amesema, katika kipindi cha uhai wake, marehemu Mafuruki  alitoa miongozo mingi kwa kampuni, hasa kipindi ilipokuwa ikipita kwenye changamoto za kiutendaji.

Dk. Inmi Patterson, Barozi wa Marekani nchini Tanzania, amemtaja marehemu Mafuruki kuwa alikuwa kisima cha hekima.

Anasema, mara kadhaa alikuwa akimshauri mambo mengi hasa wakati akifanya kazi katika mazingira ya Tanzania; na alisema, “alikuwa akinishauri wakati nafanya kazi katika mazingira yenye siasa inayobadilika haraka.“

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Gardner Habash wa Clouds Fm afariki dunia

Spread the loveALIYEKUWA mtangazaji wa kipindi cha Jahazi kinachorushwa na kituo cha...

BiasharaHabari Mchanganyiko

Wauguzi, madaktari 1000 kugawiwa mitungi ya Oryx Gas

Spread the loveKAMPUNI ya Oryx Gas na Taasisi ya Doris Mollel Foundation...

Habari Mchanganyiko

Tanzania yachaguliwa Makamu wa Rais Tume ya Shirika la Hali ya Hewa Duniani

Spread the love  TANZANIA kupitia Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA)...

Habari Mchanganyiko

NEMC yaonya wanaojenga bila tathmini ya mazingira

Spread the loveBARAZA la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC),...

error: Content is protected !!