Thursday , 2 May 2024
Home Habari Mchanganyiko EBN yatoa gari Burunge WMA kusaidia kupambana na ujangili
Habari Mchanganyiko

EBN yatoa gari Burunge WMA kusaidia kupambana na ujangili

Spread the love

KAMPUNI ya Uwindaji wa Kitalii ya EBN Hunting Safari Ltd ambayo inafanya shughuli zake katika kitalu cha uwindaji cha Hifadhi ya Jamii ya Wanyamapori ya Burunge wilayani Babati mkoani Manyara, imetoa gari aina ya Land Cruiser ili kusaidia shughuli za uhifadhi na kupambana na ujangili katika eneo la Burunge WMA. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea).

Gari hilo ambalo limegharimu Sh 205 milioni limekabidhiwa na Katibu wa EBN Hunting Safari Ltd. Charles Sylvester kwa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Babati, Anna Mbongo ambaye naye aliwakabidhi viongozi wa Burunge WMA.

Akizungumza wakati wa kukabidhi gari hilo, Sylvester amesema gari hilo ni sehemu ya makubaliano ya mkataba baina ya EBN na Burunge WMA ambapo baada ya miaka mitano gari jingine jipya litatolewa.

Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Babati, Anna Mbogo akimkabidhi kadi ya gari Mwenyekiti wa Bodi ya Burunge WMA, Patricia William. Kulia Katibu EBN Hunting Safari Ltd. Charles Sylvester.

“EBN ina imani gari hili litatumika vizuri ikiwepo kusaidia kupunguza migogoro baina ya wanyamapori na binaadamu lakini pia kukabiliana na ujangili,” amesema.

Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Babati, Mbongo kwa niaba ya Mkuu ya Mkuu wa wilaya ya Babati, Lazaro Twange alipongeza Kampuni ya EBN kwa kutekeleza makubaliano ya mkutano kwa wakati.

Amesema gari hilo pamoja na fedha nyingine ambazo zimetokewa na EBN vinapaswa kutumika vizuri kuendeleza uhifadhi na kutatua changamoto za wananchi.

“Vijiji 10 ambavyo vinaunda hifadhi hii ya Burunge vimekuwa na Maendeleo makubwa na tunaimani wananchi wataendelea kushiriki katika uhifadhi ili waendelee kunufaika,” amesema.

Meneja Mkuu wa Chemchem Association ambayo inashirikiana na EBN, Clever Zulu akisoma salamu za wakurugenzi wa EBN, amesema wanaimani kubwa kuimarika uhifadhi katika eneo hilo.

Zulu amesema EBN Hunting Safari Ltd itaendelea kushirikiana na Burunge WMA na wananchi wa Wilaya ya Babati na mkoa wa Manyara katika kuendeleza uhifadhi nakuvutia watalii zaidi.

Mwenyekiti wa Bodi ya Burunge WMA, Patricia William amesema EBN imekuwa na ushirikiano mkubwa katika kuendeleza uhifadhi na Utalii Burunge WMA na wanaimani kuendelea kupata ushirikiano mkubwa.

“Gari hili ni sehemu ya makubaliano yetu na tutatoa gari jingine na tunatarajia pia wataendelea kushirikiana na WMA katika kulinda hifadhi hiyo ili kuendeleza Utalii,” amesema.

Katibu wa Burunge WMA, Benson Mwaise amesema gari hilo litatunzwa na kuwa litasaidia katika kazi za kupunguza migogoro baina ya wanyamapori na Binaadamu lakini pia Kupambana na ujangili.

Afisa Wanyamapori wa Halmashauri ya Babati Emmanuel Laizer ameitaka Burunge WMA kutumia gari hilo kupunguza migogoro ya wanyamapori kuharibu mazao ya wananchi.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

BiasharaHabari Mchanganyiko

NMB yang’ara maonesho OSHA

Spread the loveBenki ya NMB imebeba tuzo ya kampuni bora kwenye sekta...

Habari MchanganyikoKimataifa

Ruto amteua Kahariri kuwa mkuu wa majeshi

Spread the loveRAIS wa Kenya, William Ruto, amemteua Jenerali Charles Muriu Kahariri,...

Habari Mchanganyiko

Chongolo aonya viongozi vijiji kutouza NIDA kwa wageni

Spread the loveMKUU wa Mkoa wa Songwe, Daniel Chongolo amewaonya viongozi wa...

Habari Mchanganyiko

TUCTA, OSHA wataka kampuni za madini kuiga ubunifu wa GGML

Spread the loveSHIRIKISHO la Vyama vya Wafanyakazi Tanzania (TUCTA) pamoja na Wakala...

error: Content is protected !!