Friday , 17 May 2024
Home Habari Mchanganyiko Dk. Tulia atoa somo mkutano wa Mabunge ya SADC
Habari Mchanganyiko

Dk. Tulia atoa somo mkutano wa Mabunge ya SADC

Spread the love

SPIKA wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk Tulia Ackson, amezitaka nchi za SADC kuweka nguvu kubwa katika kuhakikisha wananchi wake wanapata nishati kabla ya kuanza kufikiria nishati safi. Anaripoti Mwandishi…(endelea).

Dk. Tulia amesema nchi za Afrika hazipaswi kujilinganisha na nchi zilizoendelea ambazo zinasisitiza matumizi ya nishati safi kutokana na maendeleo ya sayansi katika nchi zao na tayari wananchi wao wote wanafikiwa na nishati.

Spika ameyasema hayo wakati akichangia Mada kuhusu mwelekeo wa upatikanaji wa nishati ya uhakika, endelevu na inayojitosheleza katika Ukanda wa Kusini mwa Afrika kwenye wa Mkutano wa 51 wa Jukwaa la Mabunge ya Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC – PF) unaoendelea katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Bingu Lilongwe nchini Malawi.

Amesisitiza kuwa Serikali za nchi wanachama zinapaswa kuzingatia uhalisia wa vyanzo vya upatikanaji wa nishati ya umeme katika nchi husika ili kukabiliana na changamoto za upatikanaji wa nishati hiyo katika eneo la kusini mwa Afrika.

“Hatuwezi kuanza kufikiria nishati endelevu wakati hata hiyo nishati wananchi hawana, uendelevu unakuwa wa kitu gani kama hakipo, hatuwezi kufikiria nishai safi waati hata hiyo chafu bado haijafikia watu wetu…ni vema kutumia rasilimali tulizo nazo kuhakikisha wananchi wetu wote wanapata nishati kisha tutakuja kuangalia namna ya kusafisha hiyo nishati,” amesema.

Amesema anatambua uwepo wa changamoto za kimazingira lakini pia uwepo wa changamoto ya ukosefu wa nishati katika nchi nyingi za SADC.

“Kama nchi nyingi za SADC bado zipo gizani, ni muhimu kutafuta suluhisho la upatikanaji wa nishati ya umeme kwa kutumia vyanzo vilivyopo ili kuwaondolea wananchi wetu changamoto hiyo,” amesema Dk. Tulia

Dk. Tulia ameainisha baadhi ya mikakati ya Serikali ya Tanzania katika kuhakikisha upatikanaji wa uhakika wa nishati ya umeme kuwa ni pamoja na mradi wa ujenzi wa bwawa la kuzalisha umeme la Mwl. Nyerere linalotarajiwa kuzalisha takribani Megawati 2115 pamoja na mradi wa ujenzi wa mitambo ya kuchakata gesi asilia kwenye kina kiferu cha bahari mkoani Lindi.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Wizara yaomba bajeti ya Sh. 67.9 bilioni, wamachinga watengewa bilioni 10

Spread the loveBAJETI ya Wizara ya maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na...

Habari MchanganyikoTangulizi

Migogoro ya ndoa yaongezeka, Serikali yawaangukia viongozi wa dini

Spread the loveMIGOGORO ya ndoa na familia imeongezeka kwa asilimia 8.3  kutoka...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Serikali yahamasisha uanzishaji vituo vya kulea watoto wachanga

Spread the loveSERIKALI imewahimiza wananchi kujenga vituo vya kulelea watoto wadogo na...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Udhibiti wa serikali wakera asasi za kiraia

Spread the loveBaadhi ya wadau wa demokrasia na viongozi wa asasi za...

error: Content is protected !!