SIMANZI. Ndivyo unavyoweza kusema baada ya mmoja wa pacha waliotenganishwa Muhimbili, Neema kufariki dunia Jumapili tarehe 10 Julai, 2022. Anaripoti Mwandishi Wetu…(endelea).
Neema amefariki dunia chini ya uangalizi maalumu ikiwa ni siku 10 tangu atenganishwe na pacha mwenzake Rehema tarehe Mosi Julai, 2022, upasuaji ambao ulielezwa kuwa na mafanikio makubwa licha ya changamoto kadhaa kutokana na namna walivyokuwa wameungana.
Taarifa hiyo imetolewa leo na Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano cha Hospitali hiyo, Aminiel Aligaesha na kueleza kuwa alifariki baada ya hali yake kubadilika badilika ghafla licha ya jitihada za madaktari.
“Nasikitika kukufahamisha kuwa mtoto Neema ambaye alitenganishwa na mwenzake Rehema amefariki jumapili ya tarehe 10 Julai saa 3 asubuhi,” amesema Aligaeshi katika taarifa yake hiyo na kuongeza;
“Akiwa ICU hali yake ilibadikika gafla, madaktari walijitahidi kurudisha hali yake bila mafanikio na hatimaye kupoteza maisha.
Taarifa hiyo haijaeleza kwa undani hali ya pacha mwingine aliyebakia zaidi ya kuleza kuwa bado yupo ICU na kutaka aendelee kuombewa.
“Twendelee kumwombea Rehema ambaye bado yupo ICU ili Mwenyezi Mungu amjalie afya njema,” amesema.
Leave a comment