Friday , 17 May 2024
Home Habari Mchanganyiko TRA yawavuta wawekezaji nchini
Habari Mchanganyiko

TRA yawavuta wawekezaji nchini

Balozi wa Kodi wa hiari Subira Mgalu akimhamasisha mfanyabiashara kuhusu faida za kutumia mashine ya EFD.
Spread the love

SERA za Mamlaka ya Mapato nchini TRA imetajwa kuwa chachu ya ongezeko la wawekezaji nchini baada ya elimu kwa mlipa kodi kuwafikia wengi wao. Anaripoti Faki Sosi, Dar es Salaam…(endelea).

Hayo yameelezwa jana tarehe 11 Julai 2022 na Subira Mgalu Balozi wa kodi nchini alipokuwa akizungumza na waandishi wa Habari alipotembelea banda la TRA kwenye maonyesho ya 49 ya sababa.

Mgalu ambaye pia ni Mbunge wa Viti Maalumu (CCM) amesema kuwa Elimu inayotolewana TRA imefumbua macho wawekezaji juu ya elimu ya mlipa kodi ambayo imewavutia wawekezaji, “kwa taarifa nimepokea wananchi wamejitokeza lakini kipekee hata wawekezaji  wemejitokeza kupata elimu ya mlipa kodi na baada ya maelezo hayo wawekezaji wamevutiwa kuwekeza nchini kwetu hili linakwenda sambamba na mpango wa Serikali ya Rais Samia Suluhu Hassan.”

Mgalu amesema ameshuhudi kitengo cha maadili cha Mamlaka hiyo ambacho kinawathibiti watumishi wa TRA ambao sio waaminifu.

Amesema  kuwa kwenye idara ya sera na utafiti ya mamlaka hiyo ambayo inatafiti namna ya kuongeza walipa kodi na kupunguza walipa kodi wachache wanaolipa kodi nyingi.

Mgalu amesema kuwa kwenye mabanda hayo ameshuhudia kitengo cha misamaha ya kodi  kwa taasisi za dini na watumishi wa serikali ambayo imeziba mianya ya watu binafsi waliokuwa wakitumia miamvuli ya dini kutolipa kodi.

Mgalu ametoa wito kwa watanzania kujifunza elimu ya kodi pia kudai lisiti kwa kila manunuzi huku wafanyabiashara wakitoa lisiti kwa kila wanapofanya mauzo.

“Kwa namna ambavyo watanzania wakielimika na tukalipa kodi , tumeanza mwaka wa fedha mpya ambao serikali inatarijia kukusana Sh41.48 trilioni ili ituletee maendeleo kwenye sekta mbalimbali.”

Amesema kuwa Mamlaka imepewa lengo la kukusanya kiasi cha Sh23 Trilioni na kwamba pesa hizo ndio zitakazojenga miradi ya kimkakati na elimu bure, utoaji wa huduma za afya na miundombinu mbalimbai nchini.

Mgalu ametoa wito kwa watanzania kuhakikisha wanapata vitambulisho vya Taifa NIDA ili kuongeza wigo wa walipa kodi kwa itakuwa na TIN namba itakayotoa tathimini walipa kodi.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Udhibiti wa serikali wakera asasi za kiraia

Spread the loveBaadhi ya wadau wa demokrasia na viongozi wa asasi za...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Nape aomba bajeti ‘kiduchu’ kwa mwaka 2024/25

Spread the loveWaziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Nape Nnauye...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Seneta: Wanasiasa hawasaidii mchakato wa Katiba mpya

Spread the loveSeneta wa jimbo la Busia, nchini Kenya, Okiya Okoiti Andrew...

Habari Mchanganyiko

Wananchi washauriwa kuongeza uelewa wa kujikinga na majanga

Spread the love WITO umetolewa kwa wananchi kuongeza uelewa na utayari kabla...

error: Content is protected !!