Friday , 17 May 2024
Home Habari Mchanganyiko Wadau wa habari wakabidhi kwa AG mapendekezo mabadiliko sheria
Habari Mchanganyiko

Wadau wa habari wakabidhi kwa AG mapendekezo mabadiliko sheria

Spread the love

WADAU wa tasnia ya habari nchini Tanzania, wamemkabidhi Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG), Jaji Eliezer Feleshi, mapendekezo yao kuhusu marekebisho ya sheria kandamizi. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam…(endelea).

Mapendekezo hayo yamekabidhiwa leo tarehe 12 Julai 2022 kwa Jaji Feleshi, na wadau hao wakiongozwa na Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF), Deodatus Balile na Makamu Mwenyekiti wa MISA-TAN, James Marenga.

Katika mapendekezo hayo, wadau hao wameshauri uundwaji wa Bodi Huru ya Ithibati ya Waandishi wa Habari, ambayo itafanya kazi ya kusikiliza malalamiko kisha kuyafanyia kazi kwa uhuru.

Wameeleza kuwa, iwapo bodi hiyo ya kitaaluma haitaingizwa mkono wa serikali katika uundwaji wake, serikali itapata sehemu ya kwenda kupeleka malalamiko yake pale itakapokwazwa na habari ama mwanahabari.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti na mwandishi wa habari leo hii jijini Dar es Salaam, wahariri hao wameeleza kwamba kuundwa kwa chombo hicho, kutakuwa mwarobaini wa malalamiko ya muda mrefu kutoka kwenye vyumba vya habari mbalimbali nchini.

Nevile Meena, Mjumbe wa Kamati Tendaji ya Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF) na Katibu Mstaafu wa taasisi hiyo amesema, iwapo serikali itaamua kuunda Bodi ya Ithibati ya Habari, basi bodi hiyo itakosa uhuru wa kufanya uamuzi pale malalamiko yatakapoihusu yenyewe (serikali).

Amesema, ili kukwepa hilo na kutenda haki kwa vyombo vyote vya habari nchini, hakuna budi kwa Bodi ya Ithibati ya Habari kuundwa na kusimamiwa na wanataaluma wenyewe ambao ndio wanahabari.

“Bodi ya Ithibati ya Habari ikisimamiwa na serikali, itakosa uhuru wa kuamua. Hiyo, bodi inapaswa kuundwa na Wanataaluma na kazi yake ni ya kitaaluma. Serikali ikiwa na malalamiko nayo inakwenda kulalamika kwenye bodi na wala haipaswi kutoa maelekezo,” ameeleza Meena.

Joseph Kulangwa, Mhariri wa Gazeti la Raia Mwema ameonesha wasiwasi iwapo serikali itasimamia uundwaji wa bodi hiyo akisema “serikali itataka wanaowaandika vizuri tu, ndio wahalalishwe kufanya kazi hiyo.”

Amesema, tasnia mbalimbali nchini zimeunda na kusimamia bodi zao wenyewe bila maelekezo ama kuingiliwa na serikali, amehoji sababu za serikali kupendekeza kuunda bodi hiyo badala ya kuwaacha wanataaluma wa habari kuunda na kusimamia bodi hiyo.

“Tasnia inatakiwa kujidhibiti yenyewe kama wanavyofanya wanasheria na wengine. Serikali ikiwa ndiye mdhibiti wa bodi hiyo, kutakuwa na upendeleo kwa magazeti so called (yanayoitwa) ya umma,” amesema Kulangwa.

Jimmy Charles, Mhariri wa Jarida la Tz & Beyond pia PANAROMA amesema, iwapo serikali itaunda bodi hiyo, itajihakikishia uhuru wa habari kutuama mikononi mwake.

“Serikali ikiunda bodi kama inavyoelekezwa na sheria, basi uhuru wa habari utaendelea kutuama kwenye mikononi yake (serikali).

“Ikumbukwe kuwa, kwa sasa serikali ndio mwamuzi wa mwisho kwa maana ya kuwa ndio mlalamikaji, msikilizaji na hakimu kwa wakati mmoja. Na ukitaka kujua hilo, utaona pale tu utakapogusa kile isichopendezwa nacho.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Udhibiti wa serikali wakera asasi za kiraia

Spread the loveBaadhi ya wadau wa demokrasia na viongozi wa asasi za...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Nape aomba bajeti ‘kiduchu’ kwa mwaka 2024/25

Spread the loveWaziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Nape Nnauye...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Seneta: Wanasiasa hawasaidii mchakato wa Katiba mpya

Spread the loveSeneta wa jimbo la Busia, nchini Kenya, Okiya Okoiti Andrew...

Habari Mchanganyiko

Wananchi washauriwa kuongeza uelewa wa kujikinga na majanga

Spread the love WITO umetolewa kwa wananchi kuongeza uelewa na utayari kabla...

error: Content is protected !!