Wednesday , 1 May 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Dk. Tulia apendekeza mbinu kumaliza mgogoro Palestina, Israel
Habari za Siasa

Dk. Tulia apendekeza mbinu kumaliza mgogoro Palestina, Israel

Spread the love

Rais wa Umoja wa Mabunge Duniani (IPU), Dk. Tulia Ackson, ameielekeza kamati inayoshughulikia masuala ya Mashariki ya Kati ya umoja huo kutembelea eneo la  Israel na Ukanda wa Gaza katika juhudi za kutafuta suluhusho linaloweza kuhakikisha amani na usalama vinapatikana. Anaripoti Mwandishi Wetu …(endelea).

Dk. Tulia ameyasema hayo leo tarehe 30 Novemba 2023 Jijini Tel Aviv nchini Israel baada ya kumaliza ziara yake ya kikazi ya siku mbili iliyompa fursa ya kukutana na kufanya mazungumzo na viongozi mbalimbali wa Israel na mamlaka ya Palestina.

 

“Nimekuja kutembelea maeneo ya Palestina na Israel ambao wote hawa mabunge yao ni wanachama wa IPU lakini muhimu zaidi kuwafahamisha kuwa tupo pamoja nao katika kipindi hiki kigumu.

“Kamati yetu inayoshughulikia masuala ya Mashariki ya Kati itakuwa hapa siku zijazo kutafuta uhalisia wa mgogoro huu na kuleta taarifa ambayo tutapata nafasi ya kuijadili ili tuone huko mbele tunakokwenda tunawezaje kuwa na amani na usalama kwa watu wote,” Dk. Tulia

Amefafanua kuwa, moja ya msingi wa IPU ni kuhakikisha uhai wa kila binadamu unalindwa na umoja huo utafanya kila linalowezekana ili dunia iwe sehemu salama na ya amani kwa binadamu wote bila kujali rangi, itikadi, imani na maeneo wanayotoka.

Aidha, amesisitiza kuwa Mpango mkakati wa umoja huo ni kuutumia Mwaka 2024 pamoja na mambo mengine kujadili kwa kina suala la amani na usalama kama ajenda muhimu kwenye mikutano yake mikuu ya mwezi Machi na Oktoba mwakani.

Katika ziara hiyo Dk. Tulia na ujumbe wake amekutana na kufanya mazungumzo na Viongozi wa Mamlaka ya Palestina Jijini Ramallah akiwemo Waziri Mkuu wa Mamlaka hiyo, Muhammad Shtayyeh pamoja na Spika wa Baraza la Mamlaka ya Palestina, Rawhi Fattouh.

Vilevile Dk. Tulia alipata fursa ya kutembelea Kijiji cha Kfar Aza Kibbutz kati ya vijiji vilivyoshambuliwa na wanamgambo wa Hamas tarehe 7 Oktoba 2023 na kufanya mazungumzo na Spika wa Bunge la Israel (Knesset), Amir Ohana, Waziri wa Kilimo na Maendeleo ya Vijiji Mhe. Avi Dicter na Wabunge Wawakilishi wa Knesset kwenye IPU walioongozwa na Danny Daddon.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Mavunde ataja malengo “Vision 2030”

Spread the loveWAZIRI wa Madini amesema dhana ya “Vision 2030” inakusudia kuiendeleza...

Habari za Siasa

Mavunde aomba bilioni 231.9 bajeti wizara ya madini

Spread the loveWAZIRI wa Madini, Anthony Mavunde leo Jumanne amewasilisha hotuba ya...

Habari za SiasaTangulizi

Lissu amjibu Fatma Karume kuhusu Rais Samia

Spread the love  MAKAMU Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema)...

Habari za SiasaTangulizi

Dk. Slaa: Watanzania iungeni mkono Chadema uchaguzi 2025

Spread the loveMWANASIASA mkongwe nchini Tanzania, Dk. Wilbroad Slaa, amewataka watanzania wakiunge...

error: Content is protected !!