RAIS wa Zanzibar, Dk. Hussein Mwinyi amewaingiza kwenye baraza lake la amwaziri Dk. Saada Mkuya Salum, Nassor Ahmed Mazrui na Omar Said Shaaban. Anaripoti Mwandishi Wetu, Zanzibar … (endelea).
Kwenye uteuzi huo leo tarehe 3 Machi 2021, Dk. Mwinyi amemteua Dk. Mkuya kuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais wa Kwanza. Dk. Mkuya aliwahi kuwa Waziri wa Fedha katika Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Mazrui ameteuliwa kuwa Waziri wa Afya, Ustawi wa Jamii, Wazee, Jinsia na Watoto huku Shaaban akiteuliwa kuwa Waziri wa Biashara na Maendeleo ya Viwanda.

Mpaka anakwaa wadhifa huo, Mazrui ni Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha ACT-Wazalendo (Zanzibar).
Kabla ya kujiunga na ACT-Wazalendo, aliwahikuwa Waziri wa Biashara na Utalii wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Naibu Katibu Mkuu Zanzibar na Mjumbe wa Baraza Kuu la Wananchi (CUF).
Taarifa iliyotolewa na Ofisi ya Katibu Mkuu Kiongozi Wateule imeelez, kwamba wateule hao wataapishwa kesho tarehe 4 Machi 2021, saa 4 asubuhi.
Leave a comment