FRANCIS Ciza maarufu Majizo, amejitokeza kumzungumzia mke wake, Elizabeth Michael ‘Lulu’ kwa uvumilivu aliouonyesha wakati wa uchumba wao na hatimaye ndoa. Anaripoti Matrida Peter, Dar es Salaam … (endelea)
Majizo ambaye ni Mmiliki wa kituo cha radio na TV ya E-FM na TV-E, alifunga pingu za maisha na Lulu, msanii wa maigizo nchini Tanzania, Jumanne ya tarehe 16 Februari 2021, katika Kanisa Katoliki la Mt. Maximilian Maria Kolbe Mwenge, Dar es Salaam.
Wawili hao walifunga pingu za maisha, baada ya kuwa kwenye mahusiano ya uchumba kwa zaidi ya miaka mitano, hali iliyoibua maneno mbalimbali, kuhusu mahusiano yao ikiwemo kuwa wameachana na mengine mengi.
Jana Jumanne, tarehe 2 Machi 2021, Majizo alitumia ukurasa wake wa Instagram, kuandika ujumbe mrefu kuzungumzia safari yake ya mahusiano hadi ndoa, huku akiambatanisha na picha iliyopigwa siku ya harusi.
Leave a comment