Wednesday , 1 May 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Dk. Biteko: Viongozi tuache alama nzuri katika utendaji wetu
Habari za Siasa

Dk. Biteko: Viongozi tuache alama nzuri katika utendaji wetu

Spread the love

Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto Biteko ametoa wito kwa viongozi mbalimbali Serikalini kuhakikisha kazi walizonazo wanazifanya kwa bidii na kuacha alama nzuri na kufaidisha wananchi. Anaripoti Mwandishi Wetu …(endelea).

Amesema hayo leo tarehe 5 Desemba 2023 wakati alipomwakilisha Rais Samia Suluhu Hassan katika Ibada Maalum ya kuaga mwili wa Baba Askofu Mstaafu, Dk. Erasto Kweka iliyofanyika katika Usharika wa Moshi Mjini mkoani Kilimanjaro.

Ibada hiyo Maalum ilihudhuriwa na viongozi mbalimbali akiwemo Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi,  Jerry Silaa na Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Nurdin Babu.

“Nikitolea mfano wa Marehemu Baba Askofu Kweka ameacha alama nzuri duniani kwani ameanzisha vitu vingi ambapo hata kama ameondoka, vitu hivyo vinaendelea kuonekana na kufaidisha wengine.

“Mfano wa enzi ya uhai wa Baba Askofu alitoa mchango mkubwa katika masuala mbalimbali ya kijamii ikiwemo kuleta usawa wa kijinsia, uanzishwaji wa miradi ya maji safi ndani na nje ya Dayosisi, Elimu, uanzishwaji wa Chama  cha Akiba na Mikopo pamoja na Benki ya Uchumi ya KKKT ambayo inawahudumia watu wote na madhehebu yote,” amesema Dk. Biteko

Dkt. Biteko ametoa wito kwa wananchi kuendelea kufanya kazi kwa bidii na kutokuta tamaa, akitolea mfano wa maisha ya Marehemu Baba Askofu Kweka ambaye alianza kutafuta maisha akiwa kijana mdogo baada ya kufiwa na baba yake akiwa na umri wa miaka 14 mpaka hatua aliyofikia sasa ya mafanikio kwa Kanisa la KKKT  na watu wanapata huduma kupitia juhudi zake.

Katika hatua nyingine, Dk. Biteko amesema Rais Samia anatambua mchango wa Marehemu Baba Askofu Kweka kwenye maendeleo ya Kanisa la KKKT na kwamba Serikali itauenzi mchango wake katika sekta pia za afya, elimu na maji.

Kwa upande wake, Mkuu wa Kanisa la Kiinjili na Kilutheri Tanzania (KKKT) na Askofu wa Dayosisi ya Kaskazini , Dk. Fredrick Onaeli Shoo amesema kuwa, viongozi wa Kanisa hilo wamefarijika na uwepo wa viongozi wa Serikali waliojumuika nao kutoka siku msiba ulipotokea mpaka wakati wa Misa hiyo Maalum.

Pia ametoa pole kwa wananchi na Serikali kufutia maafa yaliyotokea katika Wilaya ya Hanang, Mkoa wa Manyara ambapo baadhi ya wananchi wamepoteza maisha na wengine kujeruhiwa kufuatia maporomoko ya ardhi.

Ameeleza kuwa kanisa linafarijika na juhudi mbalimbali zilizochukuliwa na zinazoendelea kuchukuliwa na Serikali katika kutatua changamoto katika eneo hilo, na tayari Waziri Mkuu , Kassim Majaliwa Majaliwa yupo katika eneo la maafa na viongozi mbalimbali wa Serikali.

Marehemu Baba Askofu Mstaafu,  Dk. Erasto Kweka alizaliwa tarehe 24 Aprili, 1934 katika Kijiji cha Mamba Uswaa wilaya ya Hai mkoa wa Kilimanjaro ambapo enzi ya uhai wake alitumika katika nyanja mbalimbali ikiwemo Ualimu, kabla ya kuingia ngazi ya Utumishi wa Kanisa.

Mwaka 1973 alichaguliwa kuwa Msaidizi wa Askofu wa Dayosisi ya Kaskazini wadhifa alioutumikia hadi mwaka 1976, ambapo mwaka mmoja baadaye alichaguliwa kuwa Askofu Mkuu wa Dayosisi ya Kaskazini na pia kukaimu nafasi ya Mkuu wa Kanisa kabla ya kustaafu kwa heshima mwaka 2004.

Marehemu Baba Askofu Mstaafu, Dkt. Kweka  alifariki Jumamosi tarehe 25 Novemba, 2025  saa 4 Asubuhi  akiwa na umri wa miaka 89.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Mavunde ataja malengo “Vision 2030”

Spread the loveWAZIRI wa Madini amesema dhana ya “Vision 2030” inakusudia kuiendeleza...

Habari za Siasa

Mavunde aomba bilioni 231.9 bajeti wizara ya madini

Spread the loveWAZIRI wa Madini, Anthony Mavunde leo Jumanne amewasilisha hotuba ya...

Habari za SiasaTangulizi

Lissu amjibu Fatma Karume kuhusu Rais Samia

Spread the love  MAKAMU Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema)...

Habari za SiasaTangulizi

Dk. Slaa: Watanzania iungeni mkono Chadema uchaguzi 2025

Spread the loveMWANASIASA mkongwe nchini Tanzania, Dk. Wilbroad Slaa, amewataka watanzania wakiunge...

error: Content is protected !!